Naombeni msaada

kilungula

Member
Joined
May 6, 2014
Posts
23
Reaction score
5
Pamoja na kusoma ushauri wa tiba ya kupata haja kubwa kawaida lakini mimi bado nina tatizo hilo na linazidi. Nakunywa maji mengi ya uvuguvugu, matunda na mbogamboga, vyote hivyo havinisaidii. Nisaidieni ndugu zangu, nitumie nini. Sipendi kupata haja kwa kutumia dawa. Napenda nipate kawaida tu. Nikiingia chooni mpaka chozi linanitoka kwa kujikamua.
 
Nunua ukwaju wakutosha kama 1kg chemsha maji yachemke kabisa yatowe jikoni kisha weka huo ukwaju koroga kwa kutumia mwiko mpaka uvurugike kabisa kisha chuja kwa kutumia chujio la nazi. Upooze mpaka upoe kisha weka kwenye friji namaanisha utakuwa umepata juice yakutumia kama siku Tatu hivi. Hii ni juice kama juice nyingine utofauti ni kwamba hii inatibu constipation. Kipimo uwezo wako tu ila bora kwa asubuhi ukanywa glass moja kabla ya breakfast then baada ya nusu saa ukafungua kinywa. Jitahidi usiweke sukari komaa nao hivyohivyo na uchachu wake.

CAUTION:
Usicheze mbali na choo coz unaweza kuharisha. kuharisha huku sio ugonjwa bali unasafisha tumbo.
 
cna tofauti sana na mdau hapo juu ila naomba niongezee point kidogo,unaweza ukauchemsha ukwaju huo pamoja na maji yani vyote vichemke kwa wakati mmoja halafu ukishachuja ikipoa chota glasi moja ya juice hiyo kisha weka asali vijiko viwili,hii haina madhara yoyote kwani asali nayo ni dawa nzuri
 
Baada ya kupata hizo tiba ili tatizo lisijirudie kula kwa mpangilio huu: kunywa maji nusu saa baada ya kula na kula matunda nusu saa baada ya kula au kunywa maji,hakikisha uwe unapitisha nusu saa katika hivyo vitu.Kunywa maji lita 1.5 kila siku na usizidishe hapo.fanya mazoezi ya kukimbia au ya tumbo utakunya bila shida.
 



Majani ya Sanamaki.

Mkuu hujayanywa vizuri wewe Maji ya Uvuguvugu unakunywa mara moja kwa siku ndio unasema

hayaja kusaidia? Na hayo matunda unakula wakati gani? kula Mboga za majani Nenda Sokoni

kariakoo Kaulize Dawa moja ya kisunna inaitwa Sanamaki ni majani ya hayo Sanamaki chemsha

kwenye maji glasi 2 yachemke kama dakika 5 kisha chuja kunywa wakati wa usiku unapotaka

kwenda kulala kunywa glasi 1 kisha ulale asubuhi unapata choo hata kama choo kikiwa kigumu vipi .Na fuata pia

maagizo ya Mkuu NAMTUMBA kuhusu hiyo juisi ya ukwaju kisha uje hapa utupe feedback.



 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…