Naombeni mwongozo wakuu

Manwambele

Senior Member
Joined
Jan 4, 2016
Posts
110
Reaction score
172
Mimi ni kijana niko najishughulisha na udereva bajaji Moro, bajaji ni ya kwangu mwenyewe wala haina tajiri hesabu inapatikana 2 Mungu anasaidia lakini nina changamoto pia, zipo kama ilivyo katika kila biashara.

Sasa wakuu, nilichokuwa naomba ni msaada wa mawazo mana kuna kapesa nimepata nataka kujitanua kibiashara, kununua bajaji nyingine inashindikana mana mimi mwenywe naiona hali halisi ya usumbufu kwa madereva wenzangu wenye bajaji za mabosi pia na utunzaji hafifu.

Kwahiyo nikaamua nifikirie kununua Noah lakini nayo nkaambiwa ina changamoto nyingi tena sana.

Sasa kuna rafiki yangu yupo Dar es sallam kanishauri ninunue gari ndogo aina ya IST na mfano wa hizo niweze kufanyia Uber Dar, na mimi Dar ni mwenyeji lakini sio sana kama Moro na huduma ya Uber Moro hakuna.

Wakuu, naombeni mwongozo hapo nifanyeje au kuna mwenywe mawazo yoyote anisaidie.

Bajeti yangu ni kama Million 10.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nakushauri usifanye Biashara moja Tafadhali Biashara ya magari ina changamoto sana kwanza unaweza kupata gari mbovu na ikipata tatizo matengenezo ni ghali labda uamue Kununua gari ya chin ya milion 5 ndio uifanye ubber pia tambua madereva ni wasumbufu kuliko unavojua ukweli madereva wengi vijana wa Da'salaam haishiwi sababu mara traffic wanasumbua, sijui simu yangu inashida, Oooh wiki hii mtoto aliugua sijui nilipata matatizo ukweni, ukiletewa hesabu wiki ama mwez mmoja inayofuata ni maumivu.

Uber inalipa sana kwa madereva sio wamiliki wa magari ukiwa boss na dereva utapiga pesa nzuri. Utabadili madereva mwisho gari itachakaa na kushindwa kazi itabaki kuwa story ulinunua gari ukafanya nalo Biashara DSM ukatumia pesa ya bajaji kulitengeneza, mwisho ukafilisika ukauza bajaji ukabakiwa na gari ya DSM nayo pia ikajifia ukauza srepa Kiluvya na Kidongo Chekundu.

Ukitaka Biashara zingine fungua duka la dawa, weka maabara pesa ulionayo inatosha.

SELL or GET SOLID

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Fuata ushaur huu kijana itakusaidia sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nunua jiunge na Ubar kwani inalipa
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…