Naombeni radhi; Niliwapa pongezi Kitenge na Oscar hapa; nimejiridhisha pasipo shaka kwamba nilikosea nafuta pongeza zangu

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2019
Posts
762
Reaction score
6,984
Jana nilitoa pongezi Kwa Kitenge na Osca nikiwa nimejikita kutetea uhai wa wanadamu wenzetu pamoja na HAKI ya elimu.

Mara nyingi ninapotoa hoja napenda kujieleimisha zaidi na pale ninapobaini utofauti napenda kukiri makosa na kuepusha kuipotosha jamii. Kwa issue ya Ngorongoro Naomba kuondoa nakufuta pongezi nilizotoa baada yakuona nakujiridhosha na mambo yafuatayo;

1. Kuna viashirishia Kwa Rushwa kwenye eneo la mgogoro wa Ngorongoro ambapo viongozi wa Ndani pamoja na wageni wanahusishwa.

2. Mahakama ya Afrika ilitoa hukumu kuhusu Masai kuendelea kuishi Ngorongoro na hivyo naamini Masai wana haki na may be hata haki ya kuishi na kujiendeleza ilionekana kabla ya maamuzi

3. Mhe. RAIS alitoa maelekezo Arusha viongozi wapeleke Fedha Maendeleo na wakae na viongozi wa kimila Lakini viongozi wa serikali wamemkatalia RAIS badala yake vyombo vya Habari vya upotoshaji vimekuwa vingi. Naamini kama serikali haikumtuma Kitenge asingerusha picha na video. Means amekwenda na baraka zote. Nimejiuliza hizi baraka kazitoa Kwa Nani? Nani anamlipa? Nimeona nisimpe kichwa nisimame na ukweli wa hoja.

4. Mpango wa kuwaendeleza Wamasai nimebaini upo na hata hoja ya elimu ipo ila changamoto kubwa ni waharabu kuwaona Masai SIYO Watu. Hii imeniuma zaidi ya nilivyowaonea huruma Wamasai kuuwawa na wanyama

Niombe Tena radhi na nitoe wito Kwa wananchi kusimama na Masai. Propaganda si poa.
 
Hivi wale waarabu wa loliondo ile ni nchi ndani ya nchi? Mbona wanatesa sana watu?
 
Siungi mkono hoja zako! Uwepo wa Rushwa Serikalini isiwe sababu ya wewe kubariki balaa linaloendelea! Mwaka 1960 Ngorongoro Ilikuwa na Tembo zaidi ya 2000! Ila leo hii Tembo waliobaki ngorongoro ni 30!. Utajiri tuliopewa na Mungu duniani ni kuwa na wanyama kama hawa, na Dunia yote hadi sasa inaitegemea zaidi Tanzania maana sisi ndio wenye wanyama wengi tuliobakia duniani. Wamasai wakihamishwa ngorongoro tutakuwa tumeokoa maisha ya wanyama adimu ulimwenguni ambao wapo kwenye hatari ya kutoweka kabisa kutokana na Ongezeko na uharibifu wa binadamu. Mwaka 1959 wakati England wanasaini makubaliano na wamasai Ngorongoro ilikuwa na watu 8000! Ila hadi sasa ndani ya ngorongoro kuna makazi na na binadamu wapatao 120000! Tukiendelea na akili za ajabu baada ya miaka 50 kutoka sasa wajukuu zetu watakuja kuwa wanawaona twiga na tembo kwenye picha na I pad!. Maana wazazi Ambao ndo sisi kwa mawazo yetu haya tutawateketeza wote. Ana hekima yoyote ambae anasimama na kuwatetea fisi na chui walio kwenye hatari ya kuangamizwa ulimwenguni kutokana na uharibifu wa binadamu! #By the way kitenge awe katumwa au hajatumwa aliloongea lina Faida kwetu na kizazi kijacho! ila kwa sababu Sisi weusi huwa tunaangalia leo hatuangalii kesho, basi mimi najiandaa kurushiwa mawe na Kitenge akae chonjo maana binadamu waharibifu wasiofikiria kesho watamuwinda kama digidigi.

Shida Sio uwepo wa Masai Ngorongoro! shida ni Uharibifu unaofanywa na Binadamu Ngorongoro! (Masai Ni Binadamu) kutokana na Ungezeko lao. Kama nilivyokwambia 1959 kulikuwa na Binadamu 8000, na kulikuwa na tembo zaidi ya 2000. Leo kuna Binadamu 120000, na tembo wamebaki 30! haya ngoja binadamu wazaliane wafike 1000,000 af uje unipe idadi ya tembo waliobaki. Ushauri wangu ni binadamu wawaache wanyama Hapo mbugani Watafutiwe maeneo yatakayowafaa wao na mifugo yao. kwa usalama wa kila upande.
 
Nahitaji walinzi waambie kunanfursa njeree wapande Far express pale Karatu chap waniletee na barmaid wanne pale mto wa mbu nafungua bar .

Manjeree waachane kuwa kivutio Kama fisi hebu wake mjini bana watu gani hata hapa mjini huwezi kukuta wamepanga geto au kusikia Kuna msiba wa njeree sijawahi sijui wanakulana wale Kama mbwa mwitu 😃😃
 
Ila kusema kweli masai inabidi watoke ngorongoro kama tunahitaji kulinda hifadhi ile la sivyo after 30 years pale utakuwa mji wa kisasa wenye history ya kuwepo wanyama miaka ya nyuma
 
Siungi mkono hoja zako! Uwepo wa Rushwa Serikalini isiwe sababu ya wewe kubariki balaa linaloendelea! Mwaka 1960 Ngorongoro Ilikuwa na Tembo zaidi ya 2000! Ila leo hii Tembo waliobaki ngorongoro ni 30!. Utajiri tuliopewa na Mungu duniani ni kuwa na wanyama kama hawa, na Dunia yote hadi sasa inaitegemea zaidi Tanzania maana sisi ndio wenye wanyama wengi tuliobakia duniani. Wamasai wakihamishwa ngorongoro tutakuwa tumeokoa maisha ya wanyama adimu ulimwenguni ambao wapo kwenye hatari ya kutoweka kabisa kutokana na Ongezeko na uharibifu wa binadamu. Mwaka 1959 wakati England wanasaini makubaliano na wamasai Ngorongoro ilikuwa na watu 8000! Ila hadi sasa ndani ya ngorongoro kuna makazi na na binadamu wapatao 120000! Tukiendelea na akili za ajabu baada ya miaka 50 kutoka sasa wajukuu zetu watakuja kuwa wanawaona twiga na tembo kwenye picha na I pad!. Maana wazazi Ambao ndo sisi kwa mawazo yetu haya tutawateketeza wote. Ana hekima yoyote ambae anasimama na kuwatetea fisi na chui walio kwenye hatari ya kuangamizwa ulimwenguni kutokana na uharibifu wa binadamu! #By the way kitenge awe katumwa au hajatumwa aliloongea lina Faida kwetu na kizazi kijacho! ila kwa sababu Sisi weusi huwa tunaangalia leo hatuangalii kesho, basi mimi najiandaa kurushiwa mawe na Kitenge akae chonjo maana binadamu waharibifu wasiofikiria kesho watamuwinda kama digidigi.

Shida Sio uwepo wa Masai Ngorongoro! shida ni Uharibifu unaofanywa na Binadamu Ngorongoro! (Masai Ni Binadamu) kutokana na Ungezeko lao. Kama nilivyokwambia 1959 kulikuwa na Binadamu 8000, na kulikuwa na tembo zaidi ya 2000. Leo kuna Binadamu 120000, na tembo wamebaki 30! haya ngoja binadamu wazaliane wafike 1000,000 af uje unipe idadi ya tembo waliobaki. Ushauri wangu ni binadamu wawaache wanyama Hapo mbugani Watafutiwe maeneo yatakayowafaa wao na mifugo yao. kwa usalama wa kila upande.
I couldn't have said it better, mkuu
 
Back
Top Bottom