kufanakupona
JF-Expert Member
- Jun 18, 2015
- 522
- 421
Kwakweli umeeleza kisayansi, pia nisaidie ni sababu zipi za kibaiolojia ambazo humfanya mama mjamzto atapike?Kifupi sababu ni nyingi kutegemea na aina ya ulemavu, sasa sijui wewe unazungumzia ulemavu gani.
Ila kiujumla baadhi ni:
*matumizi ya madawa ambayo mama mjamzito hatakiwi kutumia, ikiwa ni pamoja na madawa ya asili ambayo hayajithibishwa usalama wake kisayansi. Hapa mama mjamzito akiumwa asiende tu pharmacy, aanze hospitali kwanza.
*tiba ya mionzi kwa mama mjamzito hasa katika miezi mitatu ya mwanzo ya ujauzito. Hii ni pamoja na chemotherapy kwa wenye kansa.
*upungufu wa folic acid na virutubisho vingine kwa mjamzito hasa miezi 3 ya mwanzo. Hii inamaelezo mengi muhimu maana huketa ulemavu hatari. Kifupi wajawazito watumie zile dawa wanazopewa clinic kwa uaminifu kweli, wale mboga za majani sana hasa matembele kuepuka hili tatizo.
*kurithi. Kuna baadhi ya ulemavu unahusiana na urithi tola kwa wa/mazazi au mababu.
*mtoto kukaa vibaya kwenye mfuko wa uzazi, hii huhusiana na matatizo kama ya mguu kipinda na mengine.
*magonjwa kwa mama mjamzito, hasa Syphilis, Rubella, Toxoplasmosis, na yanayohusiana na Herpes simplex virus.
*Nakadhalika.......
Maelezo hapo juu mkuuKwakweli umeeleza kisayansi, pia nisaidie ni sababu zipi za kibaiolojia ambazo humfanya mama mjamzto atapike?
Ni sababu zipi ambazo humfanya mama mjamzito abague vyakula!?
Upi ni muda mwafaka wa mama mjamzto kuanza kwenda clinic!?
Asante.
Nimekusoma vzr, ubarikiwe.Maelezo hapo juu mkuu
Shukrani sana Mkuu kwa maelezo mazuri na yanayoeleweka kirahisi.Kifupi sababu ni nyingi kutegemea na aina ya ulemavu, sasa sijui wewe unazungumzia ulemavu gani.
Ila kiujumla baadhi ni:
*matumizi ya madawa ambayo mama mjamzito hatakiwi kutumia, ikiwa ni pamoja na madawa ya asili ambayo hayajithibishwa usalama wake kisayansi. Hapa mama mjamzito akiumwa asiende tu pharmacy, aanze hospitali kwanza.
*tiba ya mionzi kwa mama mjamzito hasa katika miezi mitatu ya mwanzo ya ujauzito. Hii ni pamoja na chemotherapy kwa wenye kansa.
*upungufu wa folic acid na virutubisho vingine kwa mjamzito hasa miezi 3 ya mwanzo. Hii inamaelezo mengi muhimu maana huketa ulemavu hatari. Kifupi wajawazito watumie zile dawa wanazopewa clinic kwa uaminifu kweli, wale mboga za majani sana hasa matembele kuepuka hili tatizo.
*kurithi. Kuna baadhi ya ulemavu unahusiana na urithi tola kwa wa/mazazi au mababu.
*mtoto kukaa vibaya kwenye mfuko wa uzazi, hii huhusiana na matatizo kama ya mguu kipinda na mengine.
*magonjwa kwa mama mjamzito, hasa Syphilis, Rubella, Toxoplasmosis, na yanayohusiana na Herpes simplex virus.
*Nakadhalika.......
Shukrani sana Mkuu kwa maelezo mazuri na yanayoeleweka kirahisi.
Tafadhali, usichoke kuelemisha kuhusu suala zima la afya, afya ndiyo kitu muhimu kwa jamii. Ukipata muda tudondoshee kidogokidogo hizo hints nyingine zilizobaki.
Hapo juu umeelezea sababu za mtoto kuzaliwa mlemavu kwa kupitia mwanamke, je, zipi ni sababu za mtoto kuzaliwa mlemavu kwa kupitia mwanaume?
Doctor mimi naomba kuuliza, utamjuaje mtoto mchanga kama ana mtindio wa ubongo na je tatizo hilo linatibika ukimuwahi mapema?
Kwakweli ww n dokta, kuna imani mbalimbali katika jamii, kwamba mama akibagua chakula hiki anakuwa anazaa mtoto wa kike, ama akiwa anatapika sana anazaa mtoto wa kike, ama anapokuwa mjamzto na matiti yakawa makubwa sana napo anasemwa anazaa mtoto wa kike, miguu ikivimba napo wanasema anazaa mtoto wa kke.Mkuu mtu wa kawaida kugundua hilo mapema huwa ni kazi, japo inawezekana tangu siku ya kwanza mtoto anazaliwa, na wengi hujulikana kabla ya kufikisha mwaka mmoja.
Utagundua kwa kuona mtoto anashindwa kufanya vitu ambavyo mtoto wa kawaida wa umri wake angeweza kufanya, hii wanaita "developmental milestone" lakini hapa nitaeleza kufupi namna ya kumgundua mtoto kama ana hili tatizo kwa ku-assess (sijui ndio kutathmini) kitu kinaitwa "primitive reflexex" hivi ni vitu ambavyo mtoto mchanga anaweza kunya na endapo akifanya kinyume huashiria tatizo, vipo vingi hapa naweka vichache tu,
* kunyonya: mtoto akizaliwa hata leo akipewa ziwa vizuri anaweza nyonya hata kama sio kwa nguvu, ukiona mtoto ziwa lipo tu mdomoni hajala na hana mpango wa kunyonya ni dalili mbaya.
*kushika vitu: mtoto ukimpa kitu mkononi kwake atashika tena kwa nguvu au ukiweka kidole chako kwenye kiganya chake, sasa ukiona unaweka ila ye wala hashiki wala kuvuta ni dalili mbaya.
*kumgusa na kidole shavuni, ukifanya hivi kawaida mtoto anaweza kugeuka upande alioguswa(huhisi kuwa anapewa ziwa), ukiona hajishughulishi hata kugeuka hapo si salama sana.
*kutembea: hii huinekana vizuri kwa mtoto wa miezi 4 kuendelea, ukimsimamisha kwa kumshika na kufanya kama mnamtembeza utaona anajaribu kupiga hatua ili atembee, kinyume na hapo si dalili nzuri.
*kuanguka: mtoto mdogo angalau wa miezi 6 ukimsika kichwa chini miguu juu na kufanya kama unataka kumuangusha chini atanyoosha mikono kama anataka kujizuia asiumie, ukiona ambaye yupo yupo tu tofauti na hivyo ni dalili mbaya.
Sasa hizo ni baadhi tu, Ila si kwamba mtoto akishindwa kimoja tu kati ya hivyo basi ni tatizo, hapana, inabidi achungwe na hivyo vingine.
Naweza sema mtindio wa ubongo hautibiki ila unaweza punguzwa makali kulingana na IQ ya mtoto na dalili anazoonesha.
Tiba yao hawa ni ya kimazoezi na kitabia, pia ushauri kwa wazazi na walezi.
Mazoezi yanatengemea na umri wa mtoto, inaweza ikawa ni kucheza cheza naye, kumpa vitu achezee kwa namna ya kumfundisha, kumfundisha kula/kujilisha, kuongea, kutembea, hata kusoma na mengine kadri ya mahitaji na umri wake.
Ni mara chache dawa hutumika hasa mtoto anapoonesha dalili zaidi za magonjwa ya akili.
Vipi kuhusu:Kupitia mwanaume huwa ni ishu za kijenetic na urithi. Kumbuka kuwa mtoto huwa anarithi nusu ya alivyo kwa baba na nusu kwa mama, anachorithi mtoto ni "genes" sasa genes hizi kutoka kwa baba zinaweza kuwa zimeharibiwa "mutation" au kubadilika kiasi fulani kutokana sababu kama umri mkubwa wa baba, matumizi makubwa ya sigara na pombe, magonjwa ya kurithi kwenye ukoo wa baba, na mwisho wa siku mtoto anaweza kurithi, hata kama sio yeye kuwa mlemave basi kizazi kinachofuata.
Pia ulaji, mbegu za kiume zisizo na afya huweza kuleta mtoto mwenye matatizo, hapa nisisitizie tu mwanaume kula vyakula vyenye madini ya Zinc ya kutosha, pia vitamini B na E, hata mwezi mzima kabla ya kuingia kwenye shughuli ya kutafuta mtoto/kutungisha mimba. Mama pia atumie hivyo vitu.
NB: chanzo kizuri cha zink ni kama karanga, ufuta, mbegu za maboga, dengu na elmonds.
Hilo la miozi kama ya simu sina jibu la kisayansi, na naweza kusema haina uhusiano na ishu ya uzazi.Vipi kuhusu:
1: Mionzi ya muda mrefu inayosababishwa na kutumia kwa muda mrefu vifaa vya umeme kama simu?, haiathiri sperm za mwanaume na kupelekea kupatikana mtoto mlemavu?
2: Joto lililozidi kwenye korodani na sehemu za kiuno?, haviathiri sperm za mwanaume na kupelekea kupata mtoto mlemavu?
Hizo ni imani tu na hazina ukweli kisayansi. Na hauwezi kujua jinsia ya mtoto kwa kuangalia dalili anazoonesha mama mjamzito.Kwakweli ww n dokta, kuna imani mbalimbali katika jamii, kwamba mama akibagua chakula hiki anakuwa anazaa mtoto wa kike, ama akiwa anatapika sana anazaa mtoto wa kike, ama anapokuwa mjamzto na matiti yakawa makubwa sana napo anasemwa anazaa mtoto wa kike, miguu ikivimba napo wanasema anazaa mtoto wa kke.
Kisanyansi hayo yana ukweli wowote?
Je waweza elewa jinsia ya mtoto alieko tumboni kwa kuangalia dalili za kuona kwa macho ya kibinadam!?
Karibu kwa elimu.
Kuna mambo mawili ambayo huwa yanategemea sperm, nayo ni ugumba na kupata mtoto mlemavu. Nafikiri hayo maswali mawili niliyokuuliza hapo juu yanaweza kuapply kwenye ugumba. Hilo unalionaje Mkuu?Hilo la miozi kama ya simu sina jibu la kisayansi, na naweza kusema haina uhusiano na ishu ya uzazi.
Hilo la joto, si tatizo kwa kuwa sperm huwa zinatengezwa kila zinapohitajika (sperm ni mkusanyiko ya vitu vingi, kikubwa ni seli za uzazi), na mwili una namna ya kufanya kuendana na joto, mfano likizidi basi ngozi ya korodani hutanuka sana kuruhusu kutoa joto, na likipungua husinyaa, hii yote ni kuhakikisha kilichomo ndani hakiathiriki
Havipelekei hilo tatizo mkuu, simu wala joto.Kuna mambo mawili ambayo huwa yanategemea sperm, nayo ni ugumba na kupata mtoto mlemavu. Nafikiri hayo maswali mawili niliyokuuliza hapo juu yanaweza kuapply kwenye ugumba. Hilo unalionaje Mkuu?
Mionzi ya kutumia vifaa vya umeme kama simu kwa muda mrefu, na joto jingi maeneo ya kiuno na korodani havipelekei tatizo la ugumba?
Ahsante.
Umemaliza kila kitu Mkuu.Havipelekei hilo tatizo mkuu, simu wala joto.
sawa sawa mkuuUmemaliza kila kitu Mkuu.
Labda waje wenye maswali ya ulemavu mwingine wa watoto ambao haukutajwa hapa.
Kwa mimi, kiu yangu ya kujua visababishi vya ulemavu wa viungo kwa mtoto imeisha.