Doctor mimi naomba kuuliza, utamjuaje mtoto mchanga kama ana mtindio wa ubongo na je tatizo hilo linatibika ukimuwahi mapema?
Mkuu mtu wa kawaida kugundua hilo mapema huwa ni kazi, japo inawezekana tangu siku ya kwanza mtoto anazaliwa, na wengi hujulikana kabla ya kufikisha mwaka mmoja.
Utagundua kwa kuona mtoto anashindwa kufanya vitu ambavyo mtoto wa kawaida wa umri wake angeweza kufanya, hii wanaita "developmental milestone" lakini hapa nitaeleza kufupi namna ya kumgundua mtoto kama ana hili tatizo kwa ku-assess (sijui ndio kutathmini) kitu kinaitwa "primitive reflexex" hivi ni vitu ambavyo mtoto mchanga anaweza kunya na endapo akifanya kinyume huashiria tatizo, vipo vingi hapa naweka vichache tu,
* kunyonya: mtoto akizaliwa hata leo akipewa ziwa vizuri anaweza nyonya hata kama sio kwa nguvu, ukiona mtoto ziwa lipo tu mdomoni hajala na hana mpango wa kunyonya ni dalili mbaya.
*kushika vitu: mtoto ukimpa kitu mkononi kwake atashika tena kwa nguvu au ukiweka kidole chako kwenye kiganya chake, sasa ukiona unaweka ila ye wala hashiki wala kuvuta ni dalili mbaya.
*kumgusa na kidole shavuni, ukifanya hivi kawaida mtoto anaweza kugeuka upande alioguswa(huhisi kuwa anapewa ziwa), ukiona hajishughulishi hata kugeuka hapo si salama sana.
*kutembea: hii huinekana vizuri kwa mtoto wa miezi 4 kuendelea, ukimsimamisha kwa kumshika na kufanya kama mnamtembeza utaona anajaribu kupiga hatua ili atembee, kinyume na hapo si dalili nzuri.
*kuanguka: mtoto mdogo angalau wa miezi 6 ukimsika kichwa chini miguu juu na kufanya kama unataka kumuangusha chini atanyoosha mikono kama anataka kujizuia asiumie, ukiona ambaye yupo yupo tu tofauti na hivyo ni dalili mbaya.
Sasa hizo ni baadhi tu, Ila si kwamba mtoto akishindwa kimoja tu kati ya hivyo basi ni tatizo, hapana, inabidi achungwe na hivyo vingine.
Naweza sema mtindio wa ubongo hautibiki ila unaweza punguzwa makali kulingana na IQ ya mtoto na dalili anazoonesha.
Tiba yao hawa ni ya kimazoezi na kitabia, pia ushauri kwa wazazi na walezi.
Mazoezi yanatengemea na umri wa mtoto, inaweza ikawa ni kucheza cheza naye, kumpa vitu achezee kwa namna ya kumfundisha, kumfundisha kula/kujilisha, kuongea, kutembea, hata kusoma na mengine kadri ya mahitaji na umri wake.
Ni mara chache dawa hutumika hasa mtoto anapoonesha dalili zaidi za magonjwa ya akili.