Naombeni stori za njaa ya 1988 na Elnino ya 1998

Naombeni stori za njaa ya 1988 na Elnino ya 1998

ndege JOHN

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2015
Posts
21,643
Reaction score
51,642
Wazee wakongwe haabari zenu,

Naombeni mnisimulie stori za yaliyojiri miaka ya 1988, na wakati wa Elnino ya mwaka 1998 pamoja na na anguko la uchumi 2008 na ukata wa hela wa mwaka 2018.

Mimi njaa nasikia ni kama vita, je hali ilikuaje kipindi hicho?
 
Sawa, ebu ngoja kwanza nianze kwa kukupa tafasiri na maana halisi ya nano hili (El Nino).

Wataalamu wanaita El Nino Oscillation ni mabadiliko ya mara kwa mara ya mfumo wa anga-baharini katika Pasifiki ya kitropiki ambayo huathiri hali ya hewa ulimwenguni kote. Inatokea kila baada ya miaka 3-7 (miaka 5 kwa wastani) na kawaida hudumu miezi tisa hadi miaka miwili. Inahusishwa na mafuriko, ukame, na machafuko mengine ya ulimwengu.

Katika hali ya kawaida, au isiyo ya El Niño, upepo wa biashara hupiga magharibi pande zote za Pasifiki. Vile upepo huunganisha maji ya joto juu ya Pasifiki ya magharibi ili uso wa bahari uwe karibu na nusu mita karibu zaidi ya Indonesia kuliko karibu na Ecuador. Upandaji wa bahari unatokea mbali na pwani ya Peru na Ekvado kuleta maji baridi ya maji yenye baridi na kuongezeka kwa hifadhi. Sehemu ya magharibi ya Pasifiki ya usawa ina sifa ya hewa ya joto, ya mvua, ya chini ya shinikizo kama unyevu uliokusanywa unatumwa kwa njia ya dhoruba na mawingu.

Wakati wa tukio la ENSO, kuna ongezeko la shinikizo la hewa juu ya Bahari ya Hindi, Indonesia, na Australia, na kuanguka kwa shinikizo la hewa juu ya Tahiti na sehemu zote za Kati na Mashariki mwa Bahari ya Pasifiki. Upepo wa biashara katika Pasifiki ya kusini hupunguza au kuongoza mashariki, na maji ya joto yanaenea mashariki kutoka Pacific Magharibi na Bahari ya Hindi hadi Pasifiki ya mashariki (inafungua katika dirisha jipyamichoro na graphics za El Niño). Hii inasababisha ukame mkubwa katika Pasifiki magharibi na mvua katika Pacific kavu ya mashariki ya mashariki.

Wakati El Niño ina sifa ya joto la kawaida la bahari katikati ya Pasifiki ya mashariki ya Pasifiki, La Niña ina sifa ya joto la kawaida la bahari katika eneo hili, lakini maji ya joto katika Pasifiki magharibi. Katika miaka mingi, joto hudumu wiki chache au mwezi, baada ya hali ya hali ya hewa kurudi kwa kawaida na uvuvi inaboresha. Hata hivyo, wakati hali ya El Niño ipo kwa miezi mingi, joto kali zaidi la maji hutokea na athari zake za kiuchumi kwenye uvuvi wa ndani kwa soko la kimataifa zinaweza kuwa mbaya.
 
Be specific!
Chagua wewe simulizi ya kunipa Kama ulikuwa mkubwa 1988 nambie ile njaa ilikuaje kipindi hicho.maisha ya Watu na hofu ilikuwa kubwa kiasi gani visa gani vilitokea vikihusisha utafutaji wa chakula
 
Acha Mimi Nina experience ya 1998 nipo darasa la tatu ikatokea mzee kasimamishwa kazi jua lilikuwa Kali ardhi ni kavu kipato hakuna ilikuwa mwendo was kunywa uji kila Siku mzee akiungaunga akipata buku ananunua Mchele kitumbo tunaugombania balaa uchumi uliyumba lkn mzee alikaza kutuhudumia tukafuka kwa kweli kama ikeenda hata miaka minne binadamu na wanyama tungepotea,na kwa maisha ya dar hali ilikuwa ngumu mno baada ya jua Kali mvua ikaanza kunyesha karibu nchi nzima ilijaa maji na tukavuka kwa kweli waswahili tuliomba sana.
 
Chagua wewe simulizi ya kunipa Kama ulikuwa mkubwa 1988 nambie ile njaa ilikuaje kipindi hicho.maisha ya Watu na hofu ilikuwa kubwa kiasi gani visa gani vilitokea vikihusisha utafutaji wa chakula
Nilikuwa darasa la kwanza mwaka 1966- inawezekana hata wazazii wako walikuwa hawajazaliwa kipindi hicho, ila ninachotaka kusema ni kuwa nina kumbukumbu nyingi nzuri sana ukiniuliza vizuri!
 
Unataka sema unatabiri mojawapo kujirudia msimu huu
 
Ugali wa Yanga tumeula sana mwaka 1980's. Baada ya vita ya Uganda.
Kichuguu ukimwambia hivi anabisha.
Huo ugali wa yanga uliokula wewe ulitoka ndotoni tu kwa kuwa nina uhakika kuwa ugali wa yanga haukuwepo miaka ya themanini kwani kuaniza mwaka 1978 National Milling ilikuwa na hazina kubwa sana sana ya nafaka ikafikia hadi maafisa wa NMC wakwa ni matajiri sana kwa sababu ya rushwa waliyoanza kuhusu ngano. Hata yule jamaa aliyekuwa Mbunge wa Kahama, nadhani Jumanne Kishimba utajiri wake ulitokana na ngano ya NMC miaka hiyo.
 
Nakumbuka kabla ya njaa kulikuwa na shibe. Sasa siku moja tukiwa tunalinda ndege shambani tukaletewa chakula, baada ya kula na kushiba tukatupa ugali. Ikapita miaka kadhaa njaa ikaja. Njaa ilivyokuwa kali tukakumbuka ule ugali tuliotupa miaka kadhaa iliyopita ilibidi tirudi kuutafuta ule ugali bila mafanikio.

Hiyo njaa inanikumbusha pia zile samaki za kopo za misaada nadhani zile zilikuwa nyoka tuliletewa na mabeberu tule
 
Acha Mimi Nina experience ya 1998 nipo darasa la tatu ikatokea mzee kasimamishwa kazi jua lilikuwa Kali ardhi ni kavu kipato hakuna ilikuwa mwendo was kunywa uji kila Siku mzee akiungaunga akipata buku ananunua Mchele kitumbo tunaugombania balaa uchumi uliyumba lkn mzee alikaza kutuhudumia tukafuka kwa kweli kama ikeenda hata miaka minne binadamu na wanyama tungepotea,na kwa maisha ya dar hali ilikuwa ngumu mno baada ya jua Kali mvua ikaanza kunyesha karibu nchi nzima ilijaa maji na tukavuka kwa kweli waswahili tuliomba sana.
Nipage heshma yangu kijana...
 
Nakumbuka kabla ya njaa kulikuwa na shibe. Sasa siku moja tukiwa tunalinda ndege shambani tukaletewa chakula, baada ya kula na kushiba tukatupa ugali. Ikapita miaka kadhaa njaa ikaja. Njaa ilivyokuwa kali tukakumbuka ule ugali tuliotupa miaka kadhaa iliyopita ilibidi tirudi kuutafuta ule ugali bila mafanikio.

Hiyo njaa inanikumbusha pia zile samaki za kopo za misaada nadhani zile zilikuwa nyoka tuliletewa na mabeberu tule
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Nakumbuka kabla ya njaa kulikuwa na shibe. Sasa siku moja tukiwa tunalinda ndege shambani tukaletewa chakula, baada ya kula na kushiba tukatupa ugali. Ikapita miaka kadhaa njaa ikaja. Njaa ilivyokuwa kali tukakumbuka ule ugali tuliotupa miaka kadhaa iliyopita ilibidi tirudi kuutafuta ule ugali bila mafanikio.

Hiyo njaa inanikumbusha pia zile samaki za kopo za misaada nadhani zile zilikuwa nyoka tuliletewa na mabeberu tule
Wale samaki walikuwa wa ajabu sana,hawakuonesha kichwa wala mkia,halafu walikuwa cylindrical shape badala ya flattened shape,ulikuwa ni msaada toka Japan
 
NJAA isikieni tu, uhaba wa chakula ulitokea maeneo mengi,vyakula vya ajabuajabu vililiwa ili mradi kujaza tumbo tu.Ratiba za kula hazikueleweka,utapiamo ikawa ni kawaida tu,watoto walidumaa kwa kukosa mlo kamili.Ilikuwa ni shida kwa kweli
 
Huo ugali wa yanga uliokula wewe ulitoka ndotoni tu kwa kuwa nina uhakika kuwa ugali wa yanga haukuwepo miaka ya themanini kwani kuaniza mwaka 1978 National Milling ilikuwa na hazina kubwa sana sana ya nafaka ikafikia hadi maafisa wa NMC wakwa ni matajiri sana kwa sababu ya rushwa waliyoanza kuhusu ngano. Hata yule jamaa aliyekuwa Mbunge wa Kahama, nadhani Jumanne Kishimba utajiri wake ulitokana na ngano ya NMC miaka hiyo.
Kishimba alitajirikia kwenye dhahabu
 
Back
Top Bottom