Naombeni stori za njaa ya 1988 na Elnino ya 1998

Kishimba alitajirikia kwenye dhahabu
Alianza kwa kuuza ngano ya National milling karibu scania yote aliyouza huko Singida mwaka 1974 halafu akaangusha lori lile mtaloni karibu na milima ya Sekenke kabla hata dhahabu haijagunduluiwa huko Kahama kwani ilianza kuchimbwa mwanzoni mwa mwaka 1976 hivi. Alianza biashara kwa kununua mashine ya kusaga Unga iliyokuwa imesimikwa upande wa kuelekea Ginnery ya pamba, nafikiri eneo lile lilikuwa linaitwa Korogwe. Baada ya kuwa ameshakuwa mfanyabiashara mwenye pesa nzuri zaidi ndipo akaingilia biashara ya dhahabu na kununua miradi ya KADECO karibu yote.

Mimi namfahamu vizuri sana tangu wakati angali jamaa mwembamba mrefu sana.
 
1998 nilikua std 2,ninachokumbuka ni tukio la mama yangu na dada kukaa njiani mwezi mzima safari ya kutoka Dar kwenda ndanda kwa basi,walisimulia jinsi watu walivyopoteza maisha njiani na kuzikwa porini.
 
Nikupe mchongo?
 
Wale samaki walikuwa wa ajabu sana,hawakuonesha kichwa wala mkia,halafu walikuwa cylindrical shape badala ya flattened shape,ulikuwa ni msaada toka Japan
Hayaaaah wazee mlikula chatu hakuna samaki wa kivyo hata bunju akifora kwa sumu yake shapu ya samaki bado inabakia vile vile
 
Huo unga haukutokana na mahindi ya hapa nchini Bali ni Unga wa msaada kutoka serikali ya Marekani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…