Naombeni tafsiri ya neno 'mchepuko'

Mwenzetu

JF-Expert Member
Joined
Dec 16, 2010
Posts
550
Reaction score
194
Wajameni,nianze kwa salamu kwenu.Nimekuwa natatizwa na hili neno MCHEPUKO.Je?linawakilisha jinsia gani Kati ya MME au MKE. Naomba mnisaidie.

Mwenzetu
 
kisheria neno mchepuko lina maana ya mwanamke

kwa mwanaume ataonekana anatembea na mke watu

tufuate sheria bila shuruti
 
A.k.a side chick. Ni mwanamke au mwanaume anambaye anatembea au ana mahusiano na mwanamke au mwanaume aliyeolewa
 
A.k.a side chick. Ni mwanamke au mwanaume anambaye anatembea au ana mahusiano na mwanamke au mwanaume aliyeolewa
Neno mchepuko lilitokana na tangazo flani la ukimwi lililo sema "Acha kuchepuka baki njia kuu, michepuko sio dili" likiwa na maana wanandoa wasiende njia za pembeni yaani kuwa na wapenzi nje ya ndoa, wabaki katika ndoa ili kuilinda ndoa yao na hatari ya ukimwi. So kwa maelezo hayo mchepuko ni mtu yeyote awe me au ke anaekuwa na mahusiano ya kimapenz na mwanandoa! Yaani mfano katk ndoa mume akiwa na mahusiano na binti flan nje ya ndoa binti huyo ataitwa mchepuko, na pia mke akiwa na uhusiano na jamaa nje ya ndoa jamaa huyo ataitwa mchepuko.
 
NIMEKUELEWA MKUU KWA UFAFANUZI WAKO
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…