Naombeni tenda za kutengeneza madirisha na milango WanajamiiFroums

Naombeni tenda za kutengeneza madirisha na milango WanajamiiFroums

Moderators naomba msifutle uzi wangu labda kuhamisha kama itawezekana..

Natumai wote mnaendelea vizuri na kwa ambao mko na changamoto Mungu awafanyie wepesi mrudi kwenye hali zenu za kawaida nawaombea🤲🏽🤲🏽..

Najua sio jukwaa husika lakini nimeliweka hapa kwasababu ni jukwaa lenye wachangiaji wengi hivyo hata mods wakiamisha uzi walau muwe mmeona nilichokiandika..

Leo nitajaribu kutokujificha kidogo maana nina shida nahitaji msaada wenu, mimi ni binti ( siwezi nikasema mdogo kwasababu nina wengi ambao nimewazidi umri pia) ni mfanyakazi sector binafsi na ni mpambanaji pia sanaa, kwa baadhi wanaonifahamu nadhani wanalijua hilo… Ukiachana na kazi yangu mimi pia ni mfugaji wa Kuku wa kienyeji, nguruwe na kuku wa kisasa ambao ndo nimeanza nao round hii hapa.. Nina duka pia la Urembo, vipodozi na nguo za kike na za kiume ( Hapa nimechanganya vyote pamoja na mabegi, sendo na kila kitu, huwa naangalia upepo unavyoenda ))…. Ni kwa kifupi

Niende kwenye mada ya Leo sasa, Nilikua nina wazo la biashara ( sijui niiwekaje) lakini ni biashara kwasababu inaniingizia hela kidogo… Kuanzia mwezi wa9 mwaka jana nilikua nimetafuta vijana ambao wana ujuzi wa kutengeneza madirisha na milango ya Alminium pamoja na kazi za weldings Nikawapata, Mpaka sasa wapo almost kumi, nikafungua ofisi na tulianza kufanya baadhi ya kazi zote zimeenda vizuri, Mpaka sasa tumefanya nyingi nyingi kidogo na ninaona ina uelekeo mzuri tu hatujawahi kuharibu kazi yoyote ambayo tumepewa…

Ombi langu kwa wanaJf ambao mnaishi songea, na mlioko nje ya songea Mnipe tenda 🥹🥹, Najua humu mpo watu wengi sana mliojenga bado kuweka madirisha na mnaondelea kujenga… Naombeni mnipe kazi niwawekee madirisha na milango majumbani kwenu🙏🙏, Hata ambao mnahitaji makabati ya madukani ya vioo vya kawaida, shelves, mageti na kila kitu niwawekeeni tafadhali, Naapa sitawaangusha.. Au kwa wenye mnajenga mashule na mnahitaji madirisha na milango ya Alminium niko hapa Leejay49 naweza nikawafanyia

Pamoja na bandiko hili naweka na kazi ambazo nimezifanya, Logo Pamoja na mawasiliano yangu.. Naombeni tender wanaJf naahidi na kuapa , sitawaangusha nipo chini ya miguu yenu.. Ni binti mdogo na nina ndoto nyingi nahitaji kutimiza naomba mnisaidie🥹🙏🙏
Hongera sana kwa kazi nzuri ila humu JF karibia wote tunaishi DAR na tumeshajenga Mbweni, Masaki, Mbezi Beach na Oysterbay ivo kupata Tender ni ngumu.

Ngoja waje
 
Back
Top Bottom