Naombeni tiba ya kisaikolojia: Mwenzenu nikipanda ndege huwa nawaza hatari tupu

Naombeni tiba ya kisaikolojia: Mwenzenu nikipanda ndege huwa nawaza hatari tupu

bro kama unahc ukipanda ndege unakuwa na hofu we waagize hao cabin crew wakupe pombe unywe kwa wingi. ustukie uko airport. ikitokea imedongoka unajistukia uko mbingun au moton.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Huu ushauri huu, nimecheka balaa
 
Kabisa mkuu kwahiyo siyo ushamba
Mkuu siyo ushamba, kuna tofauti ya kupanda gari na kupanda ndege hasa hizi za kwetu, lazima zikupe mawazo na woga kidogo. Kuna phobia inatokana na heights ndio, ila mtu kuwa miles nyingi kutoka ardhini na bado hana cha kujiuliza, nadhani huo nao ni ugonjwa wa aina yake.

Sent from my TECNO K7 using JamiiForums mobile app
 
Miongoni mwa watu mliokosa raha ya adventure ni nyie mnaoogopa usafiri wa maji! Unakuta eti mtu anataka enda Zanzibar kwa ndege... ili iwe nini!!!

Kwanza meli haina uoga wowote... labda ungesema boti!!

Na kama unaenda mahali kama ZNZ, uta-ejoy zaidi ukisafiri kwa boti kuliko ukisafiri kwa meli! Kwanza meli zina ujinga wa kusafiri usiku utafikiri zimebeba wachawi!
Kikubwa ni mtu kujiandaa kiroho na kimwili, hakuna usafiri salama kivile, boat bahari ikiwa imechafuka siyo salama hata kidogo, meli nazo mara zimetoboka etc. Waliotengeneza meli ya titanic waliamini ni meli bora kabisa na ya kisasa, wakafikia hatua ya kukufuru kwa kusema "even God can't sink it". Kilichotokea ni kuwa safari yake ya kwanza tu, ilipata ajali ikakatika vipande viwili. Bottom line ni kuwa kazi ya binadamu siyo kamilifu, chochote kinaweza kutokea.

Sent from my TECNO K7 using JamiiForums mobile app
 
Mie hata lift tu napata tabu, yani huwa napanda basi tu napo hadi pawe parefu kama ni gorofa 5- napanda ngazi....


Mkuu habari ya kupanda Lift kwangu ilikuwa shida sana...... Kuna siku ikawa sina ujanja maana nilikuwa naenda ofisi fulani ambayo ipo ghorofa ya 10, hapo ikanipasa nimuombe mlinzi wa ofisini kwetu anisindikize bila kumwambia kuwa naogopa kupanda lift. Tangu siku hiyo mpaka leo uoga umeniisha, napanda lift bila hofu.
 
Samahani kwa nitakaowakwaza kwa ushamba wangu!

Mwenzenu nikipanda ndege ikiwa angani huwa naogopa ile mbaya, Hususani nikichungulia dirishani ndo kabisaa!

Vikianza Vile vihudumu vinapoelezea kuhusu maparachuti fastafasta tena kwa kingereza ....ladies and gentleman..... Huwa nasema huyu anasema nini, yaani itokee mbungi huku juu hivi vikarachuti ambavyo hata cjawahi kuvivaa ndo nivae wakati wa hatari vitasaidia kweli?

Kwanza huko angani kuelea tu ule upepo ni mtihani mkubwa KM 5 juu angani hadi ufike chini kuna mtu hapo? Balaa ufikie juu ya nguzo za umeme itakuwaje!?

Kiufupi huwa nateseka sana nikipanda ndege wakati mwingine huwa najuta kwanini nimeipanda nakuacha bus!

Kuna wakati inapokaribia kutua rubani huzima AC kusubiri kuruhusiwa kutua, basi hata kupumua huwa naona kama oksjen inapungua,

Nyie mnawezaje wenzangu! Tena comfortable kabisa huwa nawaona mnaneng'eneka kwenda hadi chooni!

Mnawezaje wenzangu? Samahan kwa hili jaman
Me mwenzako zamani nikipanda basi nikuwaga naona miti inarudi nyuma ,ila baadaye nilizoea
 
Kwenye nguzo ya umeme [emoji16][emoji16][emoji16],Mara nyingi huangukia kwenye umeme wenye msongo mkubwa na unageuka mkaa chapchap .
 
Wengine tuna phobia ya Majengo marefu pia(Sio kwamba ndio reefu,hata gorofa 3)
- elevator (ukute zile transparent )
-mteremko mkali
-Maji

Haki nna phobia nyingi mno
 
Mkuu habari ya kupanda Lift kwangu ilikuwa shida sana...... Kuna siku ikawa sina ujanja maana nilikuwa naenda ofisi fulani ambayo ipo ghorofa ya 10, hapo ikanipasa nimuombe mlinzi wa ofisini kwetu anisindikize bila kumwambia kuwa naogopa kupanda lift. Tangu siku hiyo mpaka leo uoga umeniisha, napanda lift bila hofu.
Kuna siku mtu alikua ananivuta tukapande lift, mi naogopa nimeshika chuma ananivuta yani nlikua kama ndio nimeingia mjini siku hiyo....
 
Panda na tunda, mkifika huko juu ulile kama sio kulitafuna kimasihara.
 
Kuna siku mtu alikua ananivuta tukapande lift, mi naogopa nimeshika chuma ananivuta yani nlikua kama ndio nimeingia mjini siku hiyo....
Duh! Ndo ufike juu halafu uchungulie chini unaona kama linayumba
 
uwe unakula weed before flying........utakuwa poa sana..
 
Kuna kitu kinaitwa "airplane turbulence ni shida," hapa watu huwa wanajinyea wanazimia na wengine kutoa mkojo bila taarifa, wale walioenda Brazil kutokea Dubai watanielewa! Siwezi sahau kombe la dunia 2014 Brazil.Nilipotua home hata pasipoti sikumbuki niliiweka wapi. Ukisikia bahati nasibu sijui ukishinda sijui upelekwe wapi kataa chukua hela!
Mkuu unaweza kuelezea japo kwa kifupi ilikuwaje?
 
Back
Top Bottom