Naombeni ufafanuzi kwenye hii kesi ya kugushi (Forgery)

Naombeni ufafanuzi kwenye hii kesi ya kugushi (Forgery)

Mjamaa86

JF-Expert Member
Joined
Jul 10, 2018
Posts
667
Reaction score
689
Msaada tafadhali kwa wataalamu wa sheria,

Nina rafiki yangu mzee wake (baba mzazi) amefariki mwaka Jana. Kwa sasa yeye anaishi Dar Ila kuna ndugu zake (sio wa kuzaliwa) aliwaacha wanaishi kwenye nyumba aliyojenga marehemu mzee wake iliyopo mkoani ambapo ndipo alipozikwa mzee wake.

Kosa alilofanya aliacha documents mbili ambazo yeye binafsi aliona kama hazina umuhimu sana; Moja inamtaja yeye kama mrithi ingawa alikuwa na copy yake na nyingine inawataja ndugu zake kwa kwa baba mzazi ambao hawakutajwa kama warithi. Zote izo alikuwa kazihifadhi sehemu kwenye iyo nyumba.

Ila karudi kusalimia izo documents hazipo ila kumechomekwa documents zingine mbili zinazoonyesha marehemu kauza shamba na zina muhuri wa moto ila signature ya muuzaji marehemu ndio ipo tofauti na signature halisi ya marehemu iliyopo kwenye documents zingine ambazo aliondoka nazo ikiwemo hati ya nyumba.

Sasa kwa wajuzi kwa kesi ya forgery kama hii mhusika aliyefanya kosa, mahakamani anaweza pigwa mvua ngapi?

Msaada wenu tafadhali..
 
Mkuu pole sana. je kesi imeisha funguliwa au bado? naomba uni-pm namba yako ya simu, nitakusaidia bureeeeee. asante
 
Back
Top Bottom