Ajira za Wildlife Management ni mara chache sana kuajiriwa moja kwa moja ukiwa na Bachelor kwenye hizi Taasisi, Mara chache Tanapa ndio wanapenda kuajiri moja kwa moja ambapo pia unakuta zimetolewa nafasi 10 za Bachelor ila waombaji wapo hata Elfu moja kwaiyo ni changamoto kidogo,
Mara nyingi hizi taasisi zinaajiri kada za chini kwa maana ya Basic na Technician Certificate halafu wanawaendeleza na kuja kuwa maafisa au viongozi wa baadae,Exceptional ipo kwa TFS mara nyingi ndio huajiri hao Bachelor moja kwa moja
Mwambie kijana apambane apate kwanza cheti maana MWEKA hadi mwanafunzi anamaliza pale Pesa ya Harrier New Model anakuwa ameiacha pale,
Asiangalie Serikalini tu kuna taasisi binafsi kama FZS,WWF,VIP,MWIBA,WCS na zingine nyingi zinaajiri pia tena huko ndio kuna maisha kuliko hata huku Serikalini,mimi nina jamaa yangu tulikuwa naye huku ana Diploma alipopata shavu tu huko WCS Basic salary per month ni USD 4500 bado posho na unavojua posho huwa nyingi kuliko salary