Naombeni ufahamu kuhusu kozi ya Bachelor in Wildlife and Management Tourism

Shukran[emoji120]. Naomba nitumie no zako
 
Mkuu nipo kada ya kilimo nataka nisome BSc environment studies (management) inakubalika maliasili? Vipi nafasi za kuhamia ni rahisi?, Pia ukihamia unaweza kuwa halmashauri ?
 
Mkuu nipo kada ya kilimo nataka nisome BSc environment studies (management) inakubalika maliasili? Vipi nafasi za kuhamia ni rahisi?, Pia ukihamia unaweza kuwa halmashauri ?

Kuna kipindi walikuwa wanazikubali ila hapankaribuni tena naona wamestop kuzirecognize baada ya kuona wengi wanasoma iyo kozi Open halafu wanasubmitt vyeti,

Hauwezi kuwa halmashauri labda uonbe tena kuhamia huko almashauri,hizi Taasisi au Mashirika ya Mali asili na utalii (TANAPA,NCAA,TAWA na TFS) saivi zinajitegemea kuanzia kuajiri hadi mishahara yao kwaiyo hawahusiani kabisa na Halmashauri
 
nina ndugu yangu yupo mweka anasoma degree wildlife management sasa sijui itakuwaje Mungu amsimamie kwakweli aje kupata kazi maana ada 10million afu mtu usote mtaaani kweli
 
Mimi kiko halmashauri ila kada nyingine ndio nilitaka kusoma kozi hiyo, kumbe niachane nayo asee
 
nina ndugu yangu yupo mweka anasoma degree wildlife management sasa sijui itakuwaje Mungu amsimamie kwakweli aje kupata kazi maana ada 10million afu mtu usote mtaaani kweli

Ajira za Wildlife Management ni mara chache sana kuajiriwa moja kwa moja ukiwa na Bachelor kwenye hizi Taasisi, Mara chache Tanapa ndio wanapenda kuajiri moja kwa moja ambapo pia unakuta zimetolewa nafasi 10 za Bachelor ila waombaji wapo hata Elfu moja kwaiyo ni changamoto kidogo,

Mara nyingi hizi taasisi zinaajiri kada za chini kwa maana ya Basic na Technician Certificate halafu wanawaendeleza na kuja kuwa maafisa au viongozi wa baadae,Exceptional ipo kwa TFS mara nyingi ndio huajiri hao Bachelor moja kwa moja

Mwambie kijana apambane apate kwanza cheti maana MWEKA hadi mwanafunzi anamaliza pale Pesa ya Harrier New Model anakuwa ameiacha pale,

Asiangalie Serikalini tu kuna taasisi binafsi kama FZS,WWF,VIP,MWIBA,WCS na zingine nyingi zinaajiri pia tena huko ndio kuna maisha kuliko hata huku Serikalini,mimi nina jamaa yangu tulikuwa naye huku ana Diploma alipopata shavu tu huko WCS Basic salary per month ni USD 4500 bado posho na unavojua posho huwa nyingi kuliko salary
 
shukrani mkuu
 
Well informed
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…