Naombeni ushauri jamani!

GAZETI

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2011
Posts
5,286
Reaction score
6,736
Ndugu wanajamvi heshima kwenu.
Ndugu wanajamvi naombeni ushauri juu ya jambo hili ambalo limekuwa kama mzigo kichwani kwangu. Nina rafiki zangu wawili mmoja anafanya biashara za kusafiri na huyu mwingine anafanya kazi hapa hapa Dar kitengo fulani kule bandarini. Huyu mwenzetu anayesafiri ameoa sisi wawili ni Bachelors. Lakini kuna kitu nimekigundua hivi karibuni, huyu rafiki yangu anayefanya kazi bandarini ameanzisha uhusiano na mke wa yule mwenzetu ambaye anasafiri na wote wawili yaani yule mwanamke na yule wa bandarini wameshajua kuwa nimewagundua. Najihisi kumchukia huyu rafiki yangu wa bandarini, namchukia mpaka nakosa raha lakini sijui nifanye nini! kama kuna umuhimu wa kumweleza yule rafiki yangu mwenye mke au vinginevyo naomba mnishauri ndugu zangu.
 
kabla hujamwambia mwenye mke, je nihatua gani nyingine uliyochukua?? Biblia inatuambia "onyaneni ninyi kwa ninyi" mwite mwambie anachofanya si kitu kizuri!!aache mara moja.
 
Mi naona hayakuhusu waache waendelee hilo ni bomu litalipuka tu,ila kaa mbali na huyo jamaa vunja urafiki nae.Kama hata baada ya kujuwa unafahamu uhusiano wao hawajastuka usipoteze muda kuwashauri.
 
Mi naona hayakuhusu waache waendelee hilo ni bomu litalipuka tu,ila kaa mbali na huyo jamaa vunja urafiki nae.

Hapo aliekosa adabu ni huyo mwanamke, wanawake tumejaaliwa uvumilivu sasa huyo dada kwenda kutembea na rafiki wa mumewe ni ubaradhuli na inaelekea ndio makuzi yake amezoea
 
mwite mwambie
jamaa akigundua atajua mlikuwa mpo njia moja kumbe wewe aukupendezwa pia na mambo zao
mwite mwonye mwanaume kwa wakt wake...mwite mwonye mwanamke kwa wakat wake.
wakikaidi basi fanya jitihada za kumchoresha ANAYEIBIWA ajue kwamba anaibiwa ili ujivue na LAWAMA ZAO..
 

Hili nalo neno Rose!
 

Kama unampenda (Rafiki yako) basi utamlinda.
Yapaswa uchukue hatua kulinda mali na afya ya rafiki yako
Wala usichelewe mwambie rafiki yako kuhusu mwenendo mbaya wa mke wake ila mueleze kwa tahadhali kubwa sana asije akadhani unamsukia majungu mke wake
 
Mwambie huyo jamaa 'mwizi' aache hiyo tabia haraka la sivyo utamripoti kwa jamaa... Kumbuka hata wewe ukioa atakuchukulia mkeo, labda tayari kesha tembea na mpenzi wako.
 
Ushahidi unao?
Usije ukakurupuka ukaumbuka.
Anza kuongea na hao wazinzi kwanza kabla ya mume mtu.
Tena waambie kabisa wasipoacha utamwambia rafiki yako.
Heri lawama kuliko fezea.
 
Kaa mbali sana na huyo mwanamke. Wanatabia moja, akiona unamuingila mambo yake anaweza kukuchongea kuwa ww ndo unamtongoza. Hizo kesi ziko kibao mitaani. we mshauri mshkaji wako wa bandari na umuonyeshe unakereka na hiyo hali na umweleze wazi wazi kuwa, akiendelea uvumilivu utakushinda na utaweka hadharani.
 
vijana wanasema mwite then umchane live yani kua anazingua mjamaa
 
kwanza kabla ya kumueleza ni vizur ukamwambia huyu jamaa kitendo anachokifanya co kizur na ukishamueleza yeye ndo unamueleza pia anae chukuliwa mke ni hvyo 2uu ili kurahsisha mada mana ninajua ukimueleza jamaa atachukia na akichukia huyu mwngne ataona kunatatzo kat yenu nae atataka kujua ndo unamwaga ukwel kwisha kama kwel unampenda rafik yako na familia yake fanya hvyo
 
Ongea na huyo jamaa mwizi kwanza umkanye...mwambie kabisa akiendelea utamwambia rafiki yako anayeibiwa!!!
Huyo mwenye mke kama ni rafiki yako wa kweli then umwambie hata kama utaonekana mbaya!Ni bora sasa hivi kuliko akija kugundua ulikua unajua hukumwambia mpaka akajua kwa namna nyingine!!!
 
Liz unajuwa wazinzi au unawasikia tu,huyo jamaa akienda kusema kwa hubby mke atadai huyo jamaa alimtaka akamkataa ndio maana kaja na maneno haya,ni kukaa mbali nao tu bomu litalipuka tu.
 
Dah! huyo mwanamke amekosa wanaume! adi aje kutembea na huyo rafiki w mume wake ....mke wangu nikikuta anatembea na rafik yangu naua bora nikute ni m2 nicyemfahamu.
 
Dah! huyo mwanamke amekosa wanaume! adi aje kutembea na huyo rafiki w mume wake ....mke wangu nikikuta anatembea na rafik yangu naua bora nikute ni m2 nicyemfahamu.

E bwana ee ndugu yangu unatisha, lakini nataka kukuuliza. Utamuua nani? Mkeo au rafiki yako?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…