Naombeni ushauri jinsi ya kudeal na huyu jamaa anayeniomba omba hela

📌Mpe hela yeye na demu wake alafu mtongoze huyo demu eake akijaa jipigie!!!

Hiyo ndo dawa ya mamarioo🤝
 
Kusaidia kunataka moyo sana na ni wachache wenye na moyo huo maana weengii tunachoka.
Hata mimi huwa nikimsaidia mtu ikawa kila siku ananiletea shida naanza kuona ananichukulia poa. Ila nimejifunza kujaribu kuendelea kumsaidia tu maana huena anapitia magumu kama nikiweza.
Kuna dada hapa mtaani nmeanza kumpush toka mwaka jana mwez kama wa 3 kuna muda naona kama sasa amezidi ila nakemea nafsi nasema endelea kusaidia pale unapoweza.
Sasa naona ameanza kuniambia eti mtoto wake mmoja anasema mimi ndiye ananiona kama baba yake. Hiiyo story kila sikua anairudia mimi no comment.
 
Good

Ukiweza msaidie

Huwez mwambie siwezi

Atakuelewa tu, lakini unamsaidia mtu huku umekunja roho au uonekane Bora uache,

Sikukusudia kusema lakini kipindi nipo chuo nimekaa na dgo mmoja wa dip kama unavyo jua Hawana boom kwa kipindi kile zaidi ya nyumbani.....

Lakini nilikuwa natoka na unga home, mafuta, viazi vichache nakuja kuvijazia hapa dsm na sikumtoza hata mia mpaka anaondoka mwaka + ....

Nikafanya kiroho safi baada ya kumwelewa


Nimemaliza chuo, njaa imekuja nipiga nikasaidiwa na dogo fulani kwa kipindi ambacho sina maisha oyaah mpk nikasema maybe ni kipindi kile nilimsevu chalii yule au nn so nikiwa nacho nakupa sina ntakupanga tuu kwa Leo niko empty
 
Kuna watu ukishamsaidia mara ya 1, ya 2 anaanza kukuona kama wewe una hela za kuchezea hata akiwa hana shida ya maana akikutana na wewe anaanza kutunga stori ilimradi avute mpunga.
 
Kwan hana shughuli ya kumuingizia kipato?kama hana basi jaribu kumtafutia hata vibarua walau aingize miambili Mia tatu ulizia hata kwa washkaji zako wa karibu kama kuna sehemu kuna vibarua aende akapige kazi aache kukusumbua,hapo namuonea huruma hicho kiumbe chake tu.
 
Uwe unawahi kumuomba wewe, ukiomba mara mbili tu akiwa hana ya kukupa hatokuomba tena
 
Ukimpa ww hela bureeee yeye ana offer nin kwako ,😎
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…