Naombeni ushauri juu wa watoto wangu kuacha kunyonya

Naombeni ushauri juu wa watoto wangu kuacha kunyonya

Mie nilipatwa hali kama hiyo. Nikashauriwa kutafuta papai bichi changa, unamenya then unachemsha unakunywa maji yake kila siku. Matokeo yalikuwa mazuri. Karibu na wewe. Pole sana.
 
Kuna mti unaitwa ng'wicha (kisukuma hicho) huwa unamatunda kama matiti makubwa utafute huo then uni pm mwezio nililipia pesa then takufundisha bure. Mtoto anakula mlenda na ugali😱 si bure katakuwa kasukuma ka nyumbani hako
 
Hujaiona nyota ya kijani????
Kuwa mwangalifu, huyu bado mdogo
 
Hii hali imenipata kwa watoto wangu wote huyu nilie nae akaacha kunyonya akiwa na miezi saba iliniuma sana aisee ila niliambiwa tatizo ni maziwa yanatoka kidogo kidogo hivyo inamkera Mtoto.pole sana aisee huwa natamani mwanamke aliyenamaziwa mengi ananyonyesha hadi yanamwagika dah yaani acheni.
 
Kwanza pole sana 2 tumia vyakula vya mboga hususan katika michuzi jaribu kutumia mboga ya kisambu yaani nakuonea huruma, kuna mambo haipaswi kuyazungumzia hapa ila daah siku moja mtoto wangu alikataa kunyonya hali yakua mama watoto ziwa linatoka mpaka matiti yanauma.

Ilibidi tumuone daktari, akatuandikia mashine ya kuvuta maziwa ilibidi tufanye hivyo tulitumia mashine kuvuta ziwa la mzazi na kuliweka kwenye chupa ya kunyonyea na tukampa mtoto akanyonya ziwa la mama kwa kutumia chupa ila baada ya muda alikubali kunyonya kawaida.

Hii kutonyonya mtoto husababishwa na vitu vingi moja wapo ni ladha ya ziwa lako inawezekana una upungufu wa vitamin flani sasa mtoto hua hata akinyonya haoni ladha yoyote jaribu kutumia vyakula vya mboga mboga hususan kisamvu

2. mtoto anaponyonya ikatokezea akakun'gata usimpige wala usimkemee vumilia tuu yee mara nyingi hua anaona anacheza unapomkemea kwa hasira basi ziwa hua anilikataa na ùwisho wake huliwacha kabisa
 
pole sana korino jaribu kunywa uji wa dona changanya na pilipili manga na supu ya pweza pia inasaidia kiukweli inauma sana mtoto anapokataa ziwa maana bond kati ya mtoto na mama inapungua
 
aisee hao watoto wanaokosa maziwa watakuja kuwa vilaza mno. hamna kitu muhimu kama maziwa ya mama. mimi nlinyonya mpaka maziwa ya mdogo wangu yaani mpaka nakumbuka
 
Back
Top Bottom