Kwanza pole sana 2 tumia vyakula vya mboga hususan katika michuzi jaribu kutumia mboga ya kisambu yaani nakuonea huruma, kuna mambo haipaswi kuyazungumzia hapa ila daah siku moja mtoto wangu alikataa kunyonya hali yakua mama watoto ziwa linatoka mpaka matiti yanauma.
Ilibidi tumuone daktari, akatuandikia mashine ya kuvuta maziwa ilibidi tufanye hivyo tulitumia mashine kuvuta ziwa la mzazi na kuliweka kwenye chupa ya kunyonyea na tukampa mtoto akanyonya ziwa la mama kwa kutumia chupa ila baada ya muda alikubali kunyonya kawaida.
Hii kutonyonya mtoto husababishwa na vitu vingi moja wapo ni ladha ya ziwa lako inawezekana una upungufu wa vitamin flani sasa mtoto hua hata akinyonya haoni ladha yoyote jaribu kutumia vyakula vya mboga mboga hususan kisamvu
2. mtoto anaponyonya ikatokezea akakun'gata usimpige wala usimkemee vumilia tuu yee mara nyingi hua anaona anacheza unapomkemea kwa hasira basi ziwa hua anilikataa na ùwisho wake huliwacha kabisa