Naombeni ushauri juu ya kurudi shule baada ya kuajiriwa serikalini

2025DG

JF-Expert Member
Joined
Jan 30, 2023
Posts
520
Reaction score
1,498
Habari wakuu.

Mimi kijana niliyesoma Diploma ya uuguzi na ukunga nashukuru Mungu mwaka huu nimebahatika kuajiriwa rasmi Serikali.

Nilikuwa na lengo la muda mrefu kujiendeleza kimasomo lakini nilikuwa nasubiri kwanza niingie kwa mfumo rasmi..

Wakuu naombeni ushauri wa Mambo yafuatayo.

1.Mbinu gani nitumie kurudi shule kabla ya utaratibu rasmi wa mwajiri wa miaka mitatu maana Umri unaenda na malengo binafsi.?

2.Natamani kwenda kusoma kitu tofauti na Uuguzi je hii imekaaje kiserikali kama nitabadilisha fani?

Nawasilisha
 
Mbona serikalini kuna scholarship kibao zinatolewa kwenda Asia na Ukrain pia zinakuwepo not sure after war ila zilikuwepo sana Asia,Ukrain and Russia.
Fuatilia wizarani zinatoka kila mwaka mwezi wa pili na July/september
 
Kama umri umeenda tulia tafuta pesa kwanza,kusoma watasoma hata wanao.

Shule ni lazima umtumikie mwajiri miaka mitatu ndio utapewa ruhusa ya mwajiri tofauti na hapo unatafuta matatizo bure.
Mbona Kuna watu wanarudi kabla ya hiyo miaka
 
Mbona serikalini kuna scholarship kibao zinatolewa kwenda Asia na Ukrain pia zinakuwepo not sure after war ila zilikuwepo sana Asia,Ukrain and Russia.
Fuatilia wizarani zinatoka kila mwaka mwezi wa pili na July/september
Kwa Diploma hawatoi
 
Kwa ushauri wa harakat.. hembu jiunge na chuo kikuu huria soma fani zifuatazo unaweza kubadili kazi.


1. Bachelor of social work
2.Bachelor of food science and diets
3.Uhasibu
4.IT

Kila la kheir
 
Kwa ushauri wa harakat.. hembu jiunge na chuo kikuu huria soma fani zifuatazo unaweza kubadili kazi.


1. Bachelor of social work
2.Bachelor of food science and diets
3.Uhasibu
4.IT

Kila la kheir
Asante kwa ushauri nilifikiria zaidi bachelor of science nutrition and dietetics maana hii unaweza ukasoma distance learning
 
Hapo ukitaka urahisi wa ruhusa ya kusoma kutoka kwa muajiri ni lazima usomee kozi za kujiendeleza kulingana na taaluma yako...... vinginevyo itakua gumu kupewa ruhusa
So angalia taaluma yako kama ina masomo yake ya juu
(Kisheria unatakiwa uhudumu kwa muda angalau miaka 3 kupata ruhusa ya kusoma..... lakini ukiwa ukijiongeza hata ndani ya mwaka unapata ruhusa)

Kama huipendi hiyo taaluma basi jiongeze Open University
Hapa utasoma taaluma uitakayo halafu utajuana na muajiri mbele kwa mbele kutambuliwa taaluma yako mpya na kubadilishiwa kitengo
 
Je Kama nitaenda kusoma kitu kingine tofauti na kada yangu haitaleta usumbufu kwenye kubadilisha cheo cha muundo.?
 
Nurse ina option course kama.

1.Audiology and speech pathology hii course bado HAINA muundo

2.Occupational therapy HAINA muundo kwa degree.

3Anaesthesia ni course nzuri ila changamoto yake majukumu ni mengi ya kiutendaji.

4.Bachelour of Nursing kiukweli hii course nzuri ukiwa unafundisha au research lakini sio Hospital wanawake wanaiharibu sana hii kada.
HAINA mgawanyo wa kimajukumu
 

Hongera kwa kupata nafasi ya ajira.

Njia ya mkato au ya haraka ya kwenda kusoma bila kufuata utaratibu wa kawaida kwa kweli si rahisi kupata, labda kwa njia ya kujuana sana na wakubwa....

Hata baada ya hiyo miaka mitatu au zaidi kazini kupata ruhusa ya kwenda kusoma nako mwajiri wako ataangalia kile unachotaka kukisomea kina uhitaji au manufaa kwa taasisi yake?

Kuna watu wana ndoto za kujiendeleza katika field fulani lakini mwajiri anabana kwa sababu hakuna uhitaji au faida kwa taasisi. Kwa hiyo utakuta wanamshauri akasomee kitu fulani tofauti na ndoto yake.

Kwa hiyo inategemea kama kuna uhitaji wa hicho unachotaka kukisomea katika taasisi unayoitumikia basi unaweza kupata ruhusa hiyo vinginevyo hapana.
 
Sad
 
Mkuu Mimi nilidhani kwakuwa upo field ya afya labda utakua na uanda mpana wa kuchagua kozi yoyote ya kitabibu kwa ngazi ya degree kwakuwa tayari una sifa ya diploma

Huwezi kusomea labda
Bachelor of Medical Laboratory Sciences General.
Bachelor of Pharmacy.
Bachelor of Science in Medical Imaging and Radiotherapy nk nk?
Hizo kozi ni rahisi sana kwa muajiri wako kukupa ruhusa na ukimaliza ni rahisi kubadilishiwa muuondo wako wa ajira

Kama Diploma yako inaku limit kusomea hizo kozi ulizo zitaja basi fikiria pia kufanya kozi fupi kama (NTA L4-6) ili kukupa qualification za kuapply kozi zingine za kitabibu kama nilizo zitaja hapo juu
(Sio kazi rahisi inabidi ukomae)

Shida ni pale utakapo soma mfano IT au uhasibu labda Open University halafu ukataka ubadilishiwe kitengo.... hapo unahitaji bidii na ku force kweli kweli kubadilishiwa muundo wako wa ajira vinginevyo unaweza kuishi kua na vyeti lakini ukabaki na unesi wako au labda uache kazi ukaombe kwingine kwa taaluma yako mpya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…