Naombeni ushauri juu ya kurudi shule baada ya kuajiriwa serikalini

Hizo course siruhusiwi according to TCU guide book 2024/25 Mimi ninaweza kusoma bachelor za afya kwa diploma ni kama ifuatavyo.

1.Anaesthesia.
2.Nutritional.
3.Social work.
4.physiotherapy.
5.Audiology and speech pathology.
6.Occupational therapy.
7.Katibu wa afya.

So course nyingi kwa nurse nazo ruhusiwa kusoma ni hizo zilizobaki ni za siasa.

So kwa ushauri wako itanibidi nirudi upya kusoma Diploma aisee kitu ambacho kwa Sasa sikihitaji
 
Huna sababu ya kurudi kusoma diploma ili upate nini? Soma BSc in Food, Nutrition and Dietetics
DMO atakuruhusu kwa sababu bado utakuwa kwenye afya na utaendelea kuhudumia watu hao hao

nursing kama ulivyosema hasa kwa mwanaume dah sijui nawaonaje? Manurse wamekaa
kichawa chawa sana sio wakiume sio wanawake.

Jitahidi ujikwamue huko kuna jamaa yangu alisoma hiyo BSc FND alikuwa male nurse
akabadilishiwa muungo sasa hivi ni Nutrition Officer wa hospitali ngazi ya kanda.
 
Yes. Bsc FND ina muundo mpya + Bsc CND na zote zimesajiriwa rasmi baraza la madaktari.
 
Fuata utaratibu na soma kitu kinachoendana na kada yako. Otherwise utaleta vyeti lakini hautokuwa recatecorized.

Unaweza kuleta cheti cha degree na ukaendelea kufanya kama nesi mpaka unastaafu.

Pili, fungua moyo na fanya kazi kwa moyo wote. Kumbuka msoto ulioupitia ulipokuwa unaitafuta kazi hiyo, na kuna wengi wanaitama na hawajaipata.

Ukifanya kazi hiyo hovyohovyo utajikuta mochwari mpaka unastaafu!
 

Acha tamaa - fanya kazi!
 
Inawezekana kama ulivosema ila tanguliza kusudi lako kuliko Tamaa ya kufanikiwa nkimaanisha usitake kulazimisha kusoma degree ili uje kulipwa pesa nyingi kwa kitu pia usichokipenda baadae kumbe Kuna fani nyingine za diploma nzur ambazo untafanya kazi na kuenjoy maisha Yako.....so hko utachokidomea as long as utakipenda na kukifurahia ndo kitakupa mafanikio.
Komaa September intake hyo inakuja ila jiandae kupambana na changamoto za kazini na maisha kikubwa kufikia lengo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…