Naombeni ushauri juu ya matatizo haya ya ndoa

Nakazia hapo hapo tena ikibidi atengeneze mkataba wa deni kuwa alikopa ili kuendeleza biashara, awe kama kashindwa kulipa deni kisha amuandae mdeni wake (anaemdai) aje kushikilia mali zake

Akishafirisiwa ndo atoe talaka wakishatengana anajifanya kama kaenda sehem kupambana kisha awe kama kazikomboa biashara na mke hawezi kuja kudai tena maana itakuwa kazirudisha akiwa nje ya ndoa
 
Asante Sana kwa ushauri,nitaufanyia kazi
 
safi.....Huu ushauri mzuri sana
 
Vp huyo mden wake akimgeuka nae?
 
Ndoa kwa kipigo????Hapana!Nadhani hiyo ni aina mpya ya ndoa
Sio jipya, wenzio tunadundwaga tunaambiwa tuvumilie ni kawaida. Na kaka yako ni mvumilivu ndo maana yupo na mke wake hadi sasa hivi. Tatizo ni wewe ndugu mchonganishi
 
hadi kupigwa? Mhhhh

isije kuwa mambo ya kiswahili yashamwingia

poleni sana

lakini pia huenda kuna siri ambayo mke anaijua kuhusu mali wanazochuma
 

Sio jipya, wenzio tunadundwaga tunaambiwa tuvumilie ni kawaida. Na kaka yako ni mvumilivu ndo maana yupo na mke wake hadi sasa hivi. Tatizo ni wewe ndugu mchonganishi
Ndugu tujitahidi kuwa serious(kuchukulia kwa Uzi to)matatizo ya wenzetu na kuwasaidia ikibidi!!!Hivi unaelewa kuna watu wanakabili matatizo hadi wanashindwa wafanyeje?Ndiyo maana kisaikolojia unapokuwa na tatizo mshirikishe mwenzako!Tumeshahudhuria vikao vingi vya kuwasuluhisha lakini inashindikana!Kwenye suala hili nimejifunza kitu kuwa katika ndoa suluhu ya matatizo iko mikononi mwa wanandoa wenyewe!Hata mshauri vipi,mmoja akigoma kubadilika matatizo yatabaki palepale
 
Ukiona mmesuluhisha haijawezekana ujue hakuna wa kuvunja hiyo ndoa zaidi yao wenyewe. Huyo kaka yako hadi akomeshwe vizuri ndo akili itamkaa sawa. Mtampigia kelele sana na hatawasikiliza.
Kama vipi nendeni mkareport dawati la jinsia.
.
.
We hushangai mwanaume kupigwa na mke? Kuna tatizo somewhere kwa kaka yako
 
hadi kupigwa? Mhhhh

isije kuwa mambo ya kiswahili yashamwingia

poleni sana

lakini pia huenda kuna siri ambayo mke anaijua kuhusu mali wanazochuma
Sidhani Kama kuna siri hapo!Shemeji ni mlokole walikutana kwenye kuimba kwaya!Chanzo cha utajiri ni kilimo cha Mpunga katika mashamba ya baba yetu!Nadhani chanzo cha tatizo ni hivi vikundi vya semina za kina mama!Baada kupata hiyo "elimu"kuwa mwanamke akiolewa mali zote hata zile alizomkuta nazo mume ziandikwe majina ya wote wawili mume na mke
 
Huko kwenye semina pia wanafundishwa kupiga waume zao?
Mwenye shida hapo ni bro wako. Trust me.
 
Nadhani ungeniuliza anampigaje??Kaka yangu yuko njema kwenye hiyo field,tatizo anamvizia!Hata wewe mtu akikuvizia akakumwagia maji ya moto ukiwa umekaa sebuleni bila kujiandaa au akaja na fimbo na kukushitukiza utajitetea sawa lakini hadi unafanya hivyo tayari alishakucharaza barabara!Pia kumbuka Shem anamcharaza huku anapiga kelele yeye,majirani wakija wanakuta anayelia ni mwanamke
 
Huko kwenye semina pia wanafundishwa kupiga waume zao?
Mwenye shida hapo ni bro wako. Trust me.
Kuhusu kufundishwa kupiga waume sidhani Kama iko hivyo,Ila kumbuka Shem anatumia mbinu ya kuvamia ambayo hata ungekuwa wewe huenda angekudhuru tu!Pia si kila mtu anayevumilia kipigo hawezi kupigana isipokuwa wengine wanajithibiti kwa sababu wanajua kwa hasira zao wanaweza kupigana hadi kuua
 
Wewe Ndugu mleta post, Mwachanisheni kaka yenu na huyo mwanamke wake, kama wana watoto na nyumba, Kaka yenu amwachie huyo mama na watoto ili aondokane kwenye hicho kifungo chenye jina la Ndoa, kwa kweli Ndoa haiko hivyo.
Hata kama wana hela lakini maisha ya yenye utulivu ni mazuri kuliko hilo seke seke.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…