Naombeni ushauri kabla sijafanya NECTA

Naombeni ushauri kabla sijafanya NECTA

Kaka madenge

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2021
Posts
312
Reaction score
574
Naombeni ushauri baada ya muda mrefu niliamua kuresit mtihani wa form four mwaka huu hivyo nitafanya mtihani mwezi wa 11.

Nilijiunga na Open school lakini kwa sasa hawafundishi wanatoa maswali sana tu na review na mitihani wameitoa.

Hali hii inanipa usahaulifu na kunitoa concentration kabisa

Naombeni ushauri wowote ili nipite kwenye mtihani maana shida yangu ni cheti tu.

Natanguliza shukrani zote.
 
Mm naona utataboa vizuri kuzidi hadi hapo
Mwakan soma Advance ya mwaka 1 ili usome degree hapo udom
Wazo zuri sana mkuu.

Lakini niliskia watu hii mitihani ya hivi vituo ni migumu tofauti na necta je ni kweli mkuu?
 
Wewe umeshafaulu tayari endealea tu kufanya maswali mengi uwezavyo ili ufaulu zaidi.
Nashukuru sana mkuu nitazidi kuyasolve sana naona pia muda upo mchache..
Japo pia ada wanatufukuza wengine kwa sasa
Huoni hii kama itanirudiaha nyuma kutohudhuria darasani?
 
Hakuna kitu kama hicho mitihani ni ya kawaida kinachowafelisha pc ni hawako serious na usomaji wao.
Kiukweli wengine tunajitahidi sana lakini vitu vingine vinatukwamisha
Lakini hata hivyo tunajaribu kujitahidi sana kadri ya uwezo wetu..
 
Mara nyingi shule nyingi ikifika mwezi mmoja au miwili kabla ya necta huwa wanaacha kufundisha (nyingi huwa zinakua zimemaliza syllabus) ivyo huwaacha wanafunzi kureview past papers mbalimbali, kudiscuss na kupata mda mwingi wa kujisomea. Sijaelewa unataka ufundishwe mpaka lini? Kwann usijisomee au mkatengeneza kagroup mkawa mnafundishana na kudiscuss? Ungesoma shule za serikali boarding ndo ungejua kufundishwa/kutofundishwa sio inshu saaanaa
 
Mara nyingi shule nyingi ikifika mwezi mmoja au miwili kabla ya necta huwa wanaacha kufundisha (nyingi huwa zinakua zimenaliza syllabus) ivyo huwaacha wanafunzi kureview past papers mbalimbali, kudiscuss na kupata mda mwingi wa kujisomea. Sijaelewa unataka ufundishwe mpaka lini? Kwann usijisomee au mkatengeneza kagroup mkawa mnafundishana na kudiscuss? Ungesoma shule za serikali boarding ndo ungejua kufundishwa/kutofundishwa sio inshu saaanaa
Nashukuru pia huu ni muongozo mzuri
Ni kweli topic zimekwisha kwa sasa
Wanafanya review na maswali mengi na hawafundishi sana..
 
Hayo siwezi kusema lakini mtihani wa mock niliofanya hapo shule mwezi wa 8 ulikuwa hivi
History - B
Civics - B
KiSwahili - C
Literature -D
English -C
Geography -F
Kwa kuangalia masomo yako (Arts), nashahuri uwe na tabia ya kujisomea somea sana.

Sio tu past papers, na vitabu vitabu vilivyokua recommended.

Ungekua na Mathematics kuna mwalimu ni mzoefu wa kusahihisha na kutunga NECTA ningekuunga awe anakupiga piga jamaa hana noma.
 
Hayo siwezi kusema lakini mtihani wa mock niliofanya hapo shule mwezi wa 8 ulikuwa hivi
History - B
Civics - B
KiSwahili - C
Literature -D
English -C
Geography -F
Halafu kwa nini Geography ulipata F? Yaani umelifanya somo rahisi kama hilo kuwa kama Hesabu vile!! Acha uzembe bhana.

Komaa ili kwenye huo Mtihani wako wa mwisho upate hata D tu.
 
Back
Top Bottom