Naombeni ushauri kuhusu huyu mwizi aliyepigwa Mtaani kwetu

Naombeni ushauri kuhusu huyu mwizi aliyepigwa Mtaani kwetu

Shooter Again

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2022
Posts
5,603
Reaction score
9,263
Huku mtaani kuna mwizi alichezea kichapo usiku baada ya kutuhumiwa ni mwizi na kama mnavyojua hili neno ukiitiwa usiku wa saa 7 hata kama sio mwizi raia wanapiga.

Sasa inasemekana kapona hajafa na polisi wanataka kumpitisha awatambue waliompiga na Mimi nilikua nimeenda kumshuhudia akichezea kipondo nawaza asijepata wenge akanijumuisha na Mimi kwamba nilimtembezea mkong'oto.

Nauliza hapa kama nikakamatwa na mimi natokaje kwenye huu msala wakuu sababu hapa JF ni kisima cha maarifa.

Maoni yenu muhimu wakuu
 
Mtaani kwetu ilitokeaga ishu km hiyo, kuna waliokaa maabusu miaka mitatu, achialia mbl aliepewa kesi kabisaa ambaye alikuwa mwenyekiti wa mtaa tena tokea chama upande wa pili!!😂

Mambo ya ushabiki, fwata mkumbo na kimbelembele/ kiherehere ni mambo mbaya!!

Mwanaume dhibiti mihemko yako hata wanaokuzunguka watakuja kukuomba ushauri ..
 
Ni
Huku mtaani Kuna mwizi alichezea kichapo usiku baada ya kutuhumiwa ni mwizi na kama mnavyojua hili neno ukiitiwa usiku wa saa 7 hata kama sio mwizi raia wanapiga Sasa inasemekana kapona hajafa na polisi wanataka kumpitisha awatambue waliompiga na Mimi nilikua nimeenda kumshuhudia akichezea kipondo nawaza asije pata wenge akanijumuisha na Mimi kwamba nilimtembezea mkong'oto nilikua nauliza hapa kama nikakamatwa na Mimi natokaje kwenye huu msala wakuu sababu hapa jamii forum ni kisima Cha maarifa
Ni mtaa gani ulipo ? Nione nakusaidia vipi na pia unaishi nyumba namba ngapi?
 
Back
Top Bottom