kilakitukinabuma
Member
- Jun 15, 2023
- 7
- 7
Wakuu za mida? nadhani mko poa!
Mimi ni kijana wamiaka24 nilifeli kidato cha nne mkoani huko nikawa nafanya shughuli za kilimo na washkaji zangu huko mkoani. Nilikuwa napata hela za kujikimu na chakula fresh tuu na pia kadri siku zilivyokuwa zinaenda nilikuwa nina mpango wa kulima mazao mengi ya muda mrefu na mfupi. Sikuwa na mpango wa kuja mjini kabisa kwani tangu nazaliwa hadi nabalehe sikuwahi kwenda mjini popote wala kupanda gari, nilikuwa mzee wa pori tu nilikuwa nawaona wenzangu tu wakirudi kijijini na kwenda mjini
Namlaumu mjomba wangu aliniita mjini nikamshikie kazi yake wiki moja tu aende mkoani kushughulikia mambo yake akimaliza nitaondoka kijijini na yeye ataendelea na kazi yake ya duka
Alivyorudi akawa ananishawishi nisirudi kijijini bali anitafutie gereji nikajifunze ufundi magari, dah! najuta hadi sasa kwanini nilikutana nae huyu mtu maana ndio amenipoteza maboya kabisa hadi sasa sielewi.
Nilikubali kwa jinsi alivyonishawishi na pia nilikuwa bado chalii sielewi maisha yapoje. Nikajifunza ufundi makenika chap mwaka mmoja na nusu nikaiva kiasi nikatafuta sehemu ya kulipwa nikapata sema malipo kidogo sana kitu ambacho kinapelekea kuwa tegemezi kwa ndugu kitu ambacho zamani nilikuwa sina
Kulia njaa gareji kazi hamna hadi nauli ya kurudi nyumbani nakosa wenzangu niliowaacha kijijini sasa wana familia zao washaoa.
Sasa kuna mtu anataka tufanye biashara ila kichwa hakipo tayari nahisi nina msongo wa mawazo naweza kumtia hasara maana nimechanganyikiwa siko kwenye ule ubora wangu wa zamani kabisa
Hapa nipo zangu gereji sijanywa chai wala sioni dalili ya kula mchana. Nahisi sio mimi ninayepitia mahangaiko haya
Yaani nimejifunza kazi nilioambiwa fundi hafi njaa ila naona daaa mapicha picha sijui nifanyeje yaani msingi wangu nilishakosea
Natamani miaka irudi nyuma hadi 2020 nisahihishe makosa, ila ndio hivyo tena naona nishayakanyaga tayari.