Naombeni ushauri, nataka nianze ujenzi

TEMBO WANGU

JF-Expert Member
Joined
Feb 21, 2014
Posts
930
Reaction score
1,290
Wakuu heshima kwenu! Ninakiwanja mkoa wa pwani maeneo karibu na halimashauri, ukubwa wa kiwanja no sq 600, sasa usawa wa magu ni mgumu,ila kujenga kunahitajika......nimeenda kuuliza wadau maeneo hayo wakanipa point zifuatazo

Mchanga unaweza kuchukua kwa Bibi Fulani kwa gharama 15000, kwa ndoo ndogo 200, ila wabebaji wa mchanga huo kwa ndoo wanabeba sh.200, fundi matofali anapiga tofali kwa mfuko mmoja 5000, kuhusu cement wadau wamesema nenda kiwandani kanunue tani moja wanauza jumla.sasa nawaombeni wanajf wenzangu kwa siku ya takatifu ya Jumapili, naombeni vitu vifuatavyo:

Msaada wa ramani ya vyumba vitatu, sebule, Choo cha public, jiko na stoo...naombeni free

Naombeni mnichanganulie mpaka hatua ya Boma, nitatumia tofali ngapi
Au kama una mawazo tofauti,naomba utoe ushauri wako.

Hakika utabarikiwa kwa siku ya leo,siku takatifu....kwendeni kanisani
 
Hongera Sana
Kupanga Ni Kuchagua
Vyumba Vitatu Kama Ulivyosema Ni Standard
Ninayo Ramani Nzuri Idadi Ya Vyumba 3
Haina Mbwembwe Zozote Ni Mgongo Wa Tembo
Changamoto Niko Mbali Kwenye Kutafuta Ugali
Lakini Nikirudi Home Ninaweza Kukuwekea Hapa
 
Halafu ukute Ninyi ndiyo mnalaumu graduate hawataki kujiajiri Sasa kwa mtaalamu aliyesomea kazi kwa miaka kibao ndiyo anachora ramani kwa akili na muda mwingi wewe unataka ramani ya buree daah.

Any way mtafute jamaa hapa anaitwa ellskywilly anatoa ramani za buree kwenye jukwaa hilihili.​
 
Kiwandani huanzia tani 3. Ramani just download kwa nyumba uipendayo kisha unakaa na fundi mnafanya maboresho
 
Kiwandani huanzia tani 3. Ramani just download kwa nyumba uipendayo kisha unakaa na fundi mnafanya maboresho
Kiwandani huanzia tani 30 sawa na mifuko 600. Unabeba na semi trailler.
 
Kiwandani huanzia tani 30 sawa na mifuko 600. Unabeba na semi trailler.
Tani 30 unaruhusiwa kupita nazo barabara zetu hizi? Ongeza na uzito wa semi ambao si chini ya tani saba.
 
Itakuwa vikindu huko mkuu au nakosea?
 
Tani 30 unaruhusiwa kupita nazo barabara zetu hizi? Ongeza na uzito wa semi ambao si chini ya tani saba.
Inapita highway ukitaka kupeleka ndani ndani unabeba na canter au fuso mifuko michache barabara nyingi za ndani mwisho ni tani 10 maximum
 
Tani 30 unaruhusiwa kupita nazo barabara zetu hizi? Ongeza na uzito wa semi ambao si chini ya tani saba.
Kinachoangaliwa sio uzito uliobeba, Bali pressure (mgandamizo) unauweka juu ya barabara.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…