Naombeni ushauri,nataka nikatwe mshahara uingie katika akaunti ya akiba

Masharti ya Account yapo palepale. Pitia muongozo wa bank yako na account husika. Ila kwa huduma ya standing order hutatozwa kitu. Pia pesa unaweza toa muda wowote. Maana hiyo sio fixed Account
 
Masharti ya Account yapo palepale. Pitia muongozo wa bank yako na account husika. Ila kwa huduma ya standing order hutatozwa kitu. Pia pesa unaweza toa muda wowote. Maana hiyo sio fixed Account
Anhaa.

Ndo kama ulivosema kwamba fixed account ni koasi cha pesa unaweka kwa mara moja mkupuo sio kila mwezi au siyo mkuu?
 
Yes faza exactly. Fixed amount, fixed time
naam bos lakini standing naweza katwa moja kwa moja kutoka katika mshahara pale unapoingia bila kupeleka mwenyewe,lakini tuu naweza toa mda wowote mkuu ama vipi?
 
naam bos lakini standing naweza katwa moja kwa moja kutoka katika mshahara pale unapoingia bila kupeleka mwenyewe,lakini tuu naweza toa mda wowote mkuu ama vipi?
Ndio maana yake. Hata kama unataka kumpa elfu 50 mwanao kila mwezi kama pocket money, au kama unalipa elfu 20 kila mwezi kama bill ya maji au kama unafanya saving ya laki 1 moja kila mwezi, njia ndio hiyo ya kuweka Standing order
 
Poa oa mkuu nashkuru sana kwa maelezo.mana utasema umpe wife atunze cku mbili unatumia.

Bora kuzichimbia huko benki.
Na hawana makato labda kama kila mwezi wawe wanakata alfu kadhaa kwa ushuru wa kukuwekea pesa zako kwenye bemki yao?
Au hawakati kitu ukiweka unatoa hiyo hiyo?
Ndio maana yake. Hata kama unataka kumpa elfu 50 mwanao kila mwezi kama pocket money, au kama unalipa elfu 20 kila mwezi kama bill ya maji au kama unafanya saving ya laki 1 moja kila mwezi, njia ndio hiyo ya kuweka Standing order
 
Nafikiri bank nyingi hawana monthly fee ila isipokuwa pale unapotoa fedha au miamala mingine ndio kuna Fee
 
Fixed deposit unaweka pesa at oncena sio kudunduliza et kila mwezi unaweka elfu 20

Kuna ile fixed account ukishaweka kiasi flani cha pesa hauongezi tena, unasubiria hadi kipindi ulichoamua kifike ndio unatoa pesa yote unapewa na riba. Endapo litatokea jambo ukataka kuchukua pesa yako, utapewa lakini pia utatozwa malipo ya kuvunja makubaliano.

Lakini kuna benki zina akaunti maalum ambazo unaamua kuweka kiasi flani kila mwezi na hautachukua baada ya kipindi flani. Tena benki zingine hata hiyo akaunt wewe hauifaham, wao wanachotaka hiyo tarehe ya kuhamisha pesa kutoka kwenye hiyo akaunt yako ya kawaida, pesa iwepo.

Ukifika muda mliokubaliana, pesa inawekwa kwenye akaunti yako ya kawaida.

Nafikiri lengo la mleta uzi ni hiyo ya pili.
 
Kwa Faida ya Muuliza swali
 
Ee yap yap mkuu hyo ya pili ndo ambayo nliitaka ili iniepushe na vishawishi vya kutoa toa aisee mana dah.unaweka then tatizo linatokea unatoa.

Ila hyo ukiweka unaitune mind kwamba sina changu mpaka tarehe fulani.
 
Nafikiri uwe na akaunti ya akiba (savings). Mshahara ukiingia katika checking akaunti, kiasi ulichowaambia kitatolewa tarehe fulani mfano 5 ya mwezi baada ya kupokea mshahara na k uwekwa katika akiba yako.
Fixed akaunti ni tofauti kiasi kwani unaweka kiasi fulani cha pesa na sio kila mwezi ni kwa mkupuo mmoja, halafu huzitoi kwa kipindi cha miezi ama 3, 6, 9 au 12.
Hivyo nzuri kwako ni akiba (savings) akaunti.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naa vii haiwezekani kuwaambia wakate kila inapoingia tu mkuu?

Na hyo saving unaweza toa mda wowote uutakao ama mpaka mda maalumu ambao uliuandika kwamba utatoa baada ya muda huo?
 
Naa vii haiwezekani kuwaambia wakate kila inapoingia tu mkuu?

Na hyo saving unaweza toa mda wowote uutakao ama mpaka mda maalumu ambao uliuandika kwamba utatoa baada ya muda huo?
Unaweza kuwaambia kama unajua tarehe gani mshahara unaingia katika akaunti yako na hakuna mabadiliko badiliko, kwani ni computer ndio inayofanya yote hayo.
Kutoa au kutotoa ni nidhamu yako mwenyewe, hawakuzuii kutoa unapotaka.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Anhaaa ooook mkuu nimekupata sasa,nadhani kuwa na akaunti ya akiba inaleta ari.
 

Mkuu tembelea benki ya TPB kuna huduma inaitwa WADU. Ni kwamba A/C hii ni ya akiba ambapo utasema ni shilingi ngapi ikatwe kutoka kwenye mshahara wako (kwenye source) na kuingizwa kwenye hiyo A/C kwa muda utakao utaka wewe bila Ku withdraw mfano miezi 3, 6, 9, mwaka 1 au 2 nk.

No monthly charges kwenye A/C hii na ina riba (faida) ya 5%. Ila ili uipate faida hiyo ni lazima minimum balance iwe TZS 100,000/= na kuendelea pia utii mkataba, kwamba usi withdraw kwa muda mliokubaliana
 
Iko poa ila tatizo lake ina riba,sihitajii riba kabisa mkuu,nataka nitoe kile ninachoweka tu vinginevyo nikatwe hyo gharama ya kutolea tu.
 
Nmb Wana account ya muda maalumu unaweza tumia hii account unaandika standing order kila mwezi wanatransfer pesa kwenda kwenye iyo account hautoweza toa pesa mpaka ule muda uliochagua

NB; unatakiwa ufungue acc nyingine tofauti Na iyo ya mshahara

Kingine DTB wanaproduct ambayo unaweza save kidogo kidogo kila mwezi inaitwa kibubu account kila mwezi unakatwa kiasi kile kile kinawekwa kwenye kibubu iyo pesa huwezi igusa maana unakuwa huna access nayo kabisa itarudi kwa account yako automatic bada ya maturity hivo kama ungekuwa Na account DTB nadhani hii ingekuwa best option kwako mkuu, Na hii kibubu hupewa interest ya 8% kwa miezi sita Na 10% kwa mwaka ila unaweza chagau kuanzia miezi sita mpaka Miaka mitano

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…