Naombeni ushauri nifanye nini ili nisipoteze hela zangu nilizowekeza Kenya

Naombeni ushauri nifanye nini ili nisipoteze hela zangu nilizowekeza Kenya

Alluu

Senior Member
Joined
Jan 18, 2011
Posts
127
Reaction score
142
Naombeni ushauri wa nini cha kufanya kwa haraka ili nisipoteze hela ambazo nimezituma kwa a Company in Kenya nimefanya manunuzi ya simu. Katika makubaliano ilikuwa kwamba nilipe advance/deposit ya 50% cost ya simu ili waweze kuituma na nikishaipokea hapa Dar nitalipa balance 50% iliyobaki. Sasa mimi nikafanya kama tulivyokubaliana nikapewa namba ya mpesa nikafanya international transfer na fedha ikapokelewa vizuri na huyu supplier.

Sasa baada ya muda kidogo ananiambia kuwa ili mzigo wangu upelekwe airport niweze kupokea leo Boss wake amemwambia ni lazima nilipe hela yote yaani 100% jambo ambalo limenishtua kwavile 1. Sio makubaliano yetu but 2. Siwezi kuwaamini tena, kama hiyo 50% niliyolipa advance wamebadili terms za biashara je nikimalizia balance nina uhakika gani kuwa nitatumiwa mzigo wangu? Huyu jamaa ananisisitiza nitume hela chap ili mzigo upakiwe kwenye ndege. Kwakweli nimeshtuka nimeamua kutokutuma mpaka wanieleze sababu za kubadilisha terms of business katikati ya process

Ambao mmeshafanya transactions hizi naomba ushauri wa haraka nifanye nini ili nipate either hela zangu au wanipe mzigo wangu kama tulivtokubaliana na ukishafika hapa Dar mimi nipo tayari kulipa balance cash. Maana hayo ndio yalikuwa makubaliano yetu. Nimejaribu kurudisha muamala kwa Mpesa naona mesg inakuja 'transaction failed'

Naomba ushauri wenu kwa haraka ili nisipoteze hela
 
Naombeni ushauri wa nini cha kufanya kwa haraka ili nisipoteze hela ambazo nimezituma kwa a Company in Kenya nimefanya manunuzi ya simu. Katika makubaliano ilikuwa kwamba nilipe advance/deposit ya 50% cost ya simu ili waweze kuituma na nikishaipokea hapa Dar nitalipa balance 50%
Mkuu umeibiwa...Pole.
 
Aisee mbona watu mnapigwa sana kirahisi ,kuna matapeli pia toka Zanzibar wanatumia hiyo hiyo njia kuuza simu hewa Bara
 
Nitapambana hela itarudi tu. Nitawapa mrejesho. Siwezi poteza hela kirahisi hivo. Ila katika maisha inatokea. Chamsingi unainuka unakung'uta vumbi unasonga mbele
 
Ok sawa, sio shida maadam nina mikono na afya nitapambana nitafute hela niliyoibiwa. Je kuna namna ya kufanya ili ku recover au kuzuia wengine wasiingie kwenye utapeli huu?
Kama wewe umeshindwa kuzuia kupigwa unadhani ndio utaweza zuia wengine wasipigwe. Kama walivyoweza kukurubuni wewe, na wenzio watarubuniwa hivyo hivyo.

Shukuru Mungu umebakiwa na hiyo 50%. Achana nao, ufanye maisha yako.

Ila siku nyingine kuwa makini. Pesa haitumwi kiboya kiboya bila kushika bidhaa husika mikononi mwako na kujiridhisha nayo.
 
Nitapambana hela itarudi tu. Nitawapa mrejesho. Siwezi poteza hela kirahisi hivo. Ila katika maisha inatokea. Chamsingi unainuka unakung'uta vumbi unasonga mbele
Pole sana. Ukiendelea kuishi kwa kujipa moyo hivi, basi utayashinda majaribu mengi sana maishani mwako.
 
Naombeni ushauri wa nini cha kufanya kwa haraka ili nisipoteze hela ambazo nimezituma kwa a Company in Kenya nimefanya manunuzi ya simu...
Sijasoma comments nyingine ila umeshapigwa
 
Pole mkuu, haya maswali ulitakiwa utuulize kabla, hii akili pia ulitakiwa uwe nayo kabla.

Siku zote rahisi ni gharama, ulipenda cheap matokeo yake ndio hayo. Kaa kwa kutulia jipange upya ukanunue simu dukani kwa mikono na macho yako.
 
Back
Top Bottom