Naombeni ushauri nimemfumania shemeji yangu

Ukweli huwa mzuri sana bora urafiki ufe...! Kuna kisa pale Kwenye Qoran Nabii Ibrahim Alipokuja Kumt
embelea Mwanae Ismail Akamkuta mkewe akamuuliza vipi maisha Ya hapa,amke kaanza kuongea siri za Ndani,Ibrahim akamuambia Yule Mwanamke akija mumeo Mwambie Kizingiti Hiki Hakifai...Kweli Alipokuja Ismail akaambiwa hivyo na mkewe AKAMWACHILIA MBALI...!

Sema ni mafungamano tu baadhi ya Imaan Kuweka Ugumu Ila Nikweli Mwanamke Akiwa na Tabia Chafu Achana nae tafuta Mwingine...!

MWAMBIE UKWELI NDUGU YAKO ILI UWEZE KUMNUSURU HAPO HAPAANGALII WATOTO,UMRI WA NDOA MAPENZI...!

Mke mzinifu nisimwambie rafiki yangu kwasababu gani?

Mimi niliwahi kumuona mtu kaja kutukana mtaani kisa mwanamke aliyemposa ana ukimwi hawakumuambia
 
Mambo ya ndoa humalizwa na wanandoa, usiingilie ndoa yao, utajiweka katikati ya migogoro bila sababu yoyote na mwisho wake kupoteza hata urafiki !
Kivip mkuu, yanamalizana wote wakiwa na ufahamu mzuri wa nini kinaendelea. Huyo jamaa ajue then atamaliza mwenyewe mchezo huo. Kukaa kimya ni unafiki urafiki mbaya huo.
 
Mkuu funguka,tena ufunguke kwa lengo la kumuokoa nduguyo sio kuvunja,mwambie kila kitu, muonyeshe uyajuayo theni mwachie rafiki yako aamue. Hata akikuchukia lengo lako ni zuri mkuu. Anateketea wewe unakaa kujiuliza kisa nini?
Usipofanya hivo wewe ni rafiki mnafiki,na urafiki bado utakufa maana utajiweka mbali na rafiki yako maana nafsi itakusuta sana,kwa kuwa unaujua ugonjwa anaoumwa na huwezi kumuweka wazi.
 
Unaweza kabisa kumpa hint kwamba ndugu yangu hapa kuwa makini.atajua umemaanisha nini.
Mimi huwa nasema kabisa kwa ndugu yangu ila simwambii kafanyaje mkewe.
Ndugu akibisha atakula makofi tu alafu ntakuja kumsimulia badae sana kitu kilichotokea
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…