Naombeni ushauri nina million 3 nifanye biashara gani?

Mleta mada shikilia hapa hapa. Zungukia migodini uzuri pikipiki inasafirishwa kwa bus au lori la mizigo hata ukiambiwa Runzewe kumeita wewe nenda. Usichimbe madini, wewe toa huduma ya usafirishaji au huduma nyinginezo mpaka hapo baadae uzoee utapanga mkakati mwingine.
 
Mkuu nashukuru kwa hii comment Yako imenipa mwanga
 
Fungua photo studio, ma genz wanapenda sana picha za insta na kwenye sherehe(harusi, birthday, graduu, Xmas, Eid n.k) unaenda piga vimeo picha na video na ku burn CD na nyimbo.

Pia mdau kashauri kinyozi ushauri mzuri unaweza ongezea library pia kwenye saloon, ushauri wa bucha haustoshi mtaji kupata ma friji, kukodi pango, mzigo.
 
Hii seita Iko tanga wilaya gani?
Wewe ni mdau ktk sekta ya uchimbaji?

Seita ipo mkoa wa Tanga wilaya ya Kilindi. Ukitaka kuifikia kwa wepesi, fika Gairo(Morgoro) then pale utapata noah za kukufikisha mgodini kabisa.
Huo ni mgodimama wachimbaji huwa wapungui kidogo na kuongezeka kwa wingi sana coz oparations haziishi pale.
 
1. Tengeneza account instagram
2. Uza Simu
3. Lenga watu wenye hofu ya kununua used phone au watu wanaonunua simu kwa ajili ya watu wao muhimu
4. Badilisha account iwe ya biashara
5. Tengeneza tangazo la video lenye mkono wa mwanamke
6. Tuma hiyo traffic kwenda whatsapp namba yako au profile page
7. Kama tangazo ni zuri unaanza kupata wateja ndani ya siku tatu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…