Naombeni ushauri, nyumbani kwangu nifuge mbwa au paka kama pet?

Naombeni ushauri, nyumbani kwangu nifuge mbwa au paka kama pet?

NetMaster

JF-Expert Member
Joined
Sep 12, 2022
Posts
1,454
Reaction score
4,925
Nataka nifuge pet ikiwa ni kama kiumbe alieumbwa kutoka kwa muumba alietuumba hata sisi wanadamu na vingine vilivyomo ndani ya dunia.

Nao ni viumbe kama sisi wala si wa kuchukiwa, kunyanyaswa, kudharauliwa, n.k. kufanya matendo haya mabaya kwao ni sawa na kumdharau muumba aliyewaumba aliyetuumba pia,

Wanyama nao wana haki ya furaha, kutunzwa, kutibiwa, n.k.

Nilikuwa naomba ushauri, ni yupi bora nimfuge kama pet kati ya mbwa na paka.. msosi, matibabu, malazi, naweza kumudu.

Pia vingi tunavyoviita ni makosa ya wanyama huwa ni sisi wanadamu tuliopewa akili kuzidi hivi viumbe na kupewa mamlaka ya kuvitawala ndio huwa tunakosea kwa kujigeuza madikteta, umeweka samaki nje bila kizuizi chochote na unajua kuna paka, paka alieumbwa kula samaki abambikiwe vipi kosa la wizi ?nwanadamu wamehamia sehemu na kufyeka mapori yote yaliyowalisha nyani, wanaitwaje wezi wakianza kula mazao??
 
Mkuu, kufuga paka au mbwa kama pet inakujaga automatically kwamba unakua na mapenzi na kiumbe mmoja wapo.

Wazungu unaweza kua unamdate demu afu anakuuliza "are you cat or dog person"? Yaani lazima automatically uwe unakipenda kimoja wapo.

Sasa sijui wewe unavipenda vyote au unafuga kuonesha upendo kwa wanyama au?

Kama unawapenda wote au mmoja wapo fuga, ila kama kuonesha tu upendo sikushauri ni bora uwe una donate katika mashirika/taasisi zinazo okoa wanyama na kuwafuga. Kuna moja naijua ipo Usakini unaweza ata kwenda wakakupa pet for free ukiwahakikishia kwamba atakua katika good hands na ukimchukua after muda flani wataomba picha yake.
 
Kama una pesa Fuga mbwa maana Wana vyakula adimu sana na machanjo ya maana sivyo utakuja kuzika wanapata magonjwa kibao..ila nyau anavumilia sana na vyakula vyake hata kigeto geto ni cheap..

Kingine mbwa unaweza kumfuga ana heshima sana ,ila paka ukimlea kiboss sana anajikuta yeye ndo kila kitu starehe kwa sana ipo siku utanikuta kala kitandani kwako.
 

Attachments

  • 1666873968442.jpg
    1666873968442.jpg
    66.2 KB · Views: 3
Sijawahi kumpenda paka kwa namna yoyote wanajisaidia kwenye unga alafu wanafukia siku unapikwa ugali tunaona mzigo unaelea kumbe tumesha kula unga wa juu yake kwa siku kama mbili allaullah nimemfungasha kwenye kiroba nika ponda sana fimbo nikaenda mrushia mtoni shuwani kabisa
 
Back
Top Bottom