Hope hizi zita tosha.
Watu wengi wamekuwa wakisikia nje ya mipaka ya Tanzania kuna soko kubwa la bidhaa mbali mbali zinazozalishwa nchini Tanzania lakini hawajui nini cha kufanya ili kupata wanunuzi walio nje ya Tanzania na ni hatua gani zinatakiwa kufatwa ili kuweza kuuza bidhaa nje ya nchi.
Kujiandaa kupeleka bidhaa nje: Hapa unahitaji kujua vitu vifuatavyo:
- Gharama za usajili wa bidhaa zako(Serikali kupitia shirika la viwango Tanzania imekuwa na utaratibu wa kuwasaidia wafanyabiashara kwa kutoa ushauri wa kitaalamu unaojulikana kama TAE(Technical Assistance to Exporters) na kupima bidhaa ili kuwawezesha kusafirisha nje ya nchi (export) bidhaa zilizokidhi matakwa ya viwango vya nchi zinapokwenda na kuepusha bidhaa zao kurudishwa kwa kutokidhi viwango vya nchi husika au viwango vya kitaifa.)
- Mchakato wa benki, kama unahitaji kukopa
- Kusajili bima
2. Kuelewa vya kutosha soko unalopeleka bidhaa
- Fanya utafiti wa masoko
- Tembelea ofisi mbalimbali
- Kusafiri (Kama itabidi)
3. Kupata hati stahiki
- TFDA
- TBS
- Ukaguzi wa bidhaa za mazao ya mimea n.k
4. Kukamilisha vibali na kupata ruhusa stahiki ya kuuza nje
- Wakala wa kupitisha mizigo(Muuzaji nje hulazimika kumteua wakala wa kupokea na kusafirisha mizigo (CFA) kushughulikia nyaraka zake za kutoa na kuingiza mzigo.)
- Kufungasha
- Kuweka lebo
- Kusafirisha
TARATIBU NA NYARAKA ZA KUUZA NJE
Kwa mujibu wa TRA, bidhaa za kuuza nje hazitozwi kodi na ushuru isipokuwa kwa bidhaa mbili:
- Ngozi chepe za wanyama ambazo hutozwa ushuru wa Sh600 kwa kilo.
- Korosho ghafi ambazo hutozwa dola za marekani 160 kwa tani moja ya mraba.
Utaratibu wa kushughulikia nyaraka hufanyika kwa njia ya mtandao na hukamilika kabla ya ukaguzi wa mizigo na kutoa kibali cha kusafirisha bidhaa nje ya nchi.
Mchakato wa awali huanza kwa msafirishaji mizigo nje kumteua wakala
Msafirishaji mizigo nje anakabidhi nyaraka zote ama kwa mkono au kwa njia ya kielektroniki kwa wakala ambaye naye huzipakia kwenye mtandao wa mfumo wa pamoja wa Forodha Tanzania (TANCIS) pamoja na viambatanisho vyote ikiwemo vibali kutoka idara nyingine za serikali kwenda TRA. Idara nyingine za serikali zinahakiki kibali kama kipo (System inakataa ama kudhibitisha)
Wakala hufanya utaratibu wa kushikilia nafasi ya kontena kwenye meli au kwa wakala wa usafirishaji
Upakiaji wa mzigo wa kusafirishwa nje kwenye kontena hufanyika chini ya uangalizi wa TRA na idara nyingine za serikali
Mwenye meli au wakala wa usafirishaji huwasilisha TRA taarifa za ratiba ya chombo kinachosafirisha bidhaa nje.
Ukaguzi wa TRA (Unadhibitisha au kukataa) tamko la kupakia mzigo. Tamko lililokubaliwa moja kwa moja hupelekwa kwa muongoza mitambo kama orodha ya kupakia Mzigo, na hatimaye mzigo unasubiri kupakiwa .
Ukaguzi wa kuingia getini kwa kuzingatia taratibu stahiki za ukaguzi wa geti la kituo
Getini wanawasilisha taarifa za kuingiza mzigo TRA kudhibitisha kuwasili kwa mzigo kwaajili ya kusafirishwa nje.
Nyaraka zinazohitajika
- Nyaraka zifuatazo zitatolewa kwa ajili ya kusafirisha mzigo nje ya nchi
- Ankara
- Orodha ya kufungashia
- Hati ya namba ya mlipakodi (TIN)
- Barua ya kuidhinisha
- Hati ya kusafirisha nje bidhaa kutoka mamlaka husika kutegemeana na aina ya mzigo utakaosafirishwa nje. Hati hizo ni pamoja na;
- Hati kutoka wizara ya kilimo
- Hati kutoka wizara ya nishati na madini
- Hati kutoka wizara ya utalii na maliasili
Usafirishaji wa bidhaa za chakula
Utoaji wa hati kwa ajili ya kusafirisha bidhaa nje bidhaa za vyakula kwa kawaida hufanyika pale inapohitajika au pale inapoombwa na msafirishaji bidhaa nje au nchi inayopokea bidhaa hizo. TFDA hutoa hati ya afya kwa ajili ya kuambatanishwa kwenye bidhaa za chakula zinazosafirishwa nje.
TFDA itatoa hati ya afya ikiwa imejiridhisha kuwa
- Chakula kimesajiliwa na kutengenezwa chini ya leseni ya biashara iliyotolewa na TFDA
- Kwa kampuni/watu binafsi wenye nia ya kusafirisha bidhaa nje, ukaguzi na uchukuaji wa sampuli ya mzigo utakaosafirishwa nje utafanywa na mkaguzi kabla ya kutolewa kwa hati ya afya ambapo sampuli za bidhaa husika zitafanyiwa vipimo kwa gharama za msafirishaji bidhaa nje
- Chakula husika hakikiuki kifungu chochote cha sheria ya chakula, dawa na vipodozi (TFDC Act) ya mwaka 2003, au kanuni za kuingiza chakula nchini au kukisafirisha nje ya nchi.
Taratibu za kupata kibali cha kusafirisha nje/hati ya afya;
- Mtu yeyote mwenye nia ya kusafirisha chakula kwenda nje anapaswa kuwasilisha maombi yake ya kusafirisha bidhaa hizo kwenda nje kwa mkurugenzi mkuu, TFDA.
- Barua ya maombi inapaswa kutamka kituo/bandari ya kutolea bidhaa nchini na aina ya usafiri itakayotumika. Barua hiyo iambatane na ankara kifani inayoonyesha
- Jina na anwani ya kampuni inayosafirisha bidhaa nje
- Jina na anwani ya anayeingiza bidhaa hizo kwenye nchi inayokwenda
- Kiasi na thamani ya bidhaa za chakula zitakazosafirishwa nje
- Aina ya matini ya kufungashia
- Jina la mtengenezaji
- Nchi bidhaa zinapokwenda
Maombi yaambatane na ada ya kuyashughulikia kama ilivyoainishwa kwenye kanuni ya ada na tozo mbalimbali ya mwaka 2011. Baada ya ukaguzi wa nyaraka na kuridhishwa na taarifa zilizowasilishwa, hati ya afya/kibali cha kusafirisha bidhaa nje hutolewa kwa msafirishaji. Kibali hicho kitakuwa na uhalali kwa muda wa miezi mitatu kuanzia tarehe ya siku kilipotolewa na kitatumika mara moja pekee.