Naombeni ushauri wa biashara ya Bodaboda

Butiyangu

Senior Member
Joined
May 19, 2018
Posts
123
Reaction score
168
Mm ni mjasiliamari mtarajiwa, natarajia kuanzisha biashara ya kukodisha pikipiki Kwa mkataba. Natarajia kuanza na pikipiki 10 ambazo nitawapatia vijana walio katika vikundi.

Nitawapatia Kwa mkataba wa miezi kumi na tatu, na baada ya hapo pikipiki itakuwa Mali yake, mfumo wa biashara hii nataka niufanye Kwa njia ya kuwa na kampuni.

Sasa naomba ushauri Kwa watalaam na wadau wenye uzoefu na biashara hii wanipe mawazo yao ya namna ya kufungua kampuni ya Aina hiyo. Pia utaratibu wa kisheria katika biashara ya Aina hiyo.
 
Swali: Umeshawahi kuwa boda boda? Kama hujawahi usifanye hiyo biashara maana Huijui.
 
Mimi si mtaalamu wa masuala ya biashara na ili kupata ushauri wa kitaalam unaweza kukutana na wataalam waliosajiliwa. Ila naweza kusema haya nilisikia watu wakisema hii biashara sio nikajifariji kwamba control yangu ni nzuri na tofauti na wanaofanyia mazoea kilichonikuta ni siri yangu hadi sasa nimebaki na baadhi ya pikpik nimefungia ndani.

Hii ni aina ya biashara ambayo ili uifanye itakubidi muda wote uwekeze hapo huwezi kufanya mambo mengine. vijana wanaoendesha vyombo hivyo ndo watakukwamisha ile hujuwahi ona. tena wewe unaanza na kumi..

Jiangalie vizuri mkuu.. ni rahisi kusimamia fulo moja ya kubeba mawe,mchanga etc kuliko toyo 10. ila akili kichwani mwako kama unaamini kwenye mipango yako basi kila la heri.
 
Hapo sijakuelewa vizuri, hiyo biashara ulikuwa unafanya Kwa stail gani? Ulikuwa unawapatia Kwa mkataba au kuwakodishia
 
Sikukatishi tamaa ingia mtaani fanya utafiti uone...kama unawekeza kwenye usafiri wa aina hiyo ebu jaribu kununua bajaji alafu katia bima kubwa... Lakini pikipiki kila kichochoro zipo, wengine wanaendesha na usiku alafu vijiwe vingi vya hawa vijana siyo waaminifu ukora mwingi... Mi nipo hapa arusha lakini sioni raha wala unafuu wa hii kitu sijui pikipiki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…