Naombeni ushauri wa kibiashara

tembocard

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2018
Posts
247
Reaction score
121
Habari zenu naombeni mnishauri nmetengeneza Contena kubwa la saiz ya chumba kimoja cha saizi sasa nmefikiria biashara ya kufanya kwenye ilo contena ila kuna mtu kanipa wazo kuwa nilipeleke maeneo ya ng'ong'ona udom nilifanye salon ya kiume ndo Bdo nafikiria ilo wazo, naombeni wakuu na nyie mnisaidie mawazo yenu juu ya hili natanguliza shukrani
 
Set karibu na taasisi za elimu kama chuo kikuu, weka glossary, uza vyakula vya kubeba
 
lisogeze hadi kwenye msongamano wa watu wenye kipato cha kati. (buguruni, ilala, sinza, tabata n.k) weka umeme kwenye container lako tafuta majiko stahiki tafuta wajuzi narudia tafuta wajuzi wa kupika fungua biashara ya baga na chips, jikite zaidi kwenye packaging (take away nzuri). huna haja ya kuweka viti nje, mwaga kokoto nje kwenye eneo lako na weka meza moja ndefu (angalia picha). Lete mrejesho baadae
 

Attachments

  • bar table.jpg
    2.8 KB · Views: 39
Asante
 
Uza fresh juice, smoothie, maziwa moto baridi pamoja na bites! Ongezea na mahitaji km pads_ sabun za kuogea, kufulia, maji ya kunywa,n.k
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…