Naombeni ushauri wa kisheria kwa hili

Naombeni ushauri wa kisheria kwa hili

Mabrek

Senior Member
Joined
Sep 17, 2013
Posts
125
Reaction score
21
habarini wana jamiiforums, poleni na majukumu ,ombi langu ni kutaka kupata ushauri kwa hili ninamdogo wangu wa kiume ni mtumishi serikalin ,kwa bahati mbaya alikuwa anauhusiano wa kimapenzi na mwanafunzi wa kidato cha tatu kuelekea kidato cha nne na akampa ujauzito,ndugu wa huyo binti walikuja juu xana kiasi cha kumpiga binti kumlazimisha amtaje muhusika lakni binti aligoma katu katu kutaja, japo mdogo wangu aliendelea kutoa huduma zote muhm kisiri mpaka akajifungua na anamtoto wa miezi minne lakini mazingira anayoishi ni magumu mno kimaisha lengo letu ni kutaka kumchukua na ikiwezekana amuoe,xaxa hofu yetu kubwa tukijionesha kwa ndugu zake wanaweza tufungulia kesi? au vyovyote xo tunaomba ushauri kwa hli tufanyaje,asanten
 
Mkuu Mabrek,natafuta kwanza nukta kwenye bandiko lako. Halafu,xo ndio nini? Wewe na mdogo wako,kwa uandishi huu,mkubwa nani? Ha ha ha ha

Mkuu,jazia mada yako ili ushauriwe. Mosi,mwanafunzi alikuwa na umri gani wakati akipewa ujauzito? Pili,umepita muda gani tangu jambo hilo litokee?

Kimsingi,kumpa mwanafunzi mimba ni kosa la jinai. Laweza kuwa kosa la ubakaji kama msichana yuko chini ya miaka 18. Pia,hapo kunatendeka kosa la kusababisha kuachisha masomo.

Mkuu Mabrek,kosa la jinai halina ukomo isipokuwa mhusika akifariki. Namshauri mdogo wako abakie mafichoni.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu hapo hamna kesi hata mkulu wa kaya alisema ni viherehere vyao wenyewe!
 
ok samahan kwa uandishi ambao haukutimia binti ana umri wa miaka 20 na mpaka sasa ana mtoto wa miez minne
 
Kama bint ana umri wa miaka 20 sasa hivi ambapo ana mtoto wa miezi minne, yumkini alipata ujauzito akiwa na zaidi ya miaka 18. Kama jibu ni ndio, basi ndugu yako hana kosa ikiwa tu tendo la kufanya naye ngono iliyosababisha mimba hiyo lilikuwa lina hiyari ya bint.
Je, kwa bint kuzaa, kumesababisha asisitishe masomo yake? Kama ni ndio basi kona kosa hapo la kumsababishia binti asimalize masomo yake. Nitafanya upekuzi wa sheria iliyovunjwa na adhabu zake.

Kaka.
 
asante kaka.kumbe mambo bado magumu kiasi hicho? ni bora kutembea kwa mguu kutoka tanzania mpaka zambia kuliko kwenda jela;
 
Faten sheria za nchi.... MPE pole sana huyo Dada aliyepigwa. Jaman women are treated badly . msaada mzur Wa kukusaidia ni nyie kusoma sheria na kujipeleka mahakaman. Mlichokifanya sio kizur alafu mnataka msaada Wa kisheria? Labda msaada Wa kukamatwa....
 
Kama keshajifungua basi nendeni tu mkajitambulishe na mseme nia yenu
 
Ukimpa mwanafunzi mimba kesi ipo mpaka mwezi wa nane kipindi mtoto yupo tumbon na akisha jifunguwa hapo hamna kesi jmh cha kufanya mkapime D.N.A chukueni toto lenu kiroho safi sema mtapigwa faini ukwen kuwen tayar kwa hilo.
 
Mi natafuta kosa silioni,hakuna mzazi ataweza kukupeleka mahakama eti kisa mzazi wa mjukuu wao kajitokeza!hapo kma ni kesi ya ubakaji mpka sasa haina ushaidi wa kutosha,mwambie dogo ajitokeze tu akamlee mwanae,
 
habarini wana jamiiforums, poleni na majukumu ,ombi langu ni kutaka kupata ushauri kwa hili ninamdogo wangu wa kiume ni mtumishi serikalin ,kwa bahati mbaya alikuwa anauhusiano wa kimapenzi na mwanafunzi wa kidato cha tatu kuelekea kidato cha nne na akampa ujauzito,ndugu wa huyo binti walikuja juu xana kiasi cha kumpiga binti kumlazimisha amtaje muhusika lakni binti aligoma katu katu kutaja, japo mdogo wangu aliendelea kutoa huduma zote muhm kisiri mpaka akajifungua na anamtoto wa miezi minne lakini mazingira anayoishi ni magumu mno kimaisha lengo letu ni kutaka kumchukua na ikiwezekana amuoe,xaxa hofu yetu kubwa tukijionesha kwa ndugu zake wanaweza tufungulia kesi? au vyovyote xo tunaomba ushauri kwa hli tufanyaje,asanten
Ushauri ni mdogo wako atangulie segerea akakutane na wanaume huko ili na yeye wamharibie maisha. Pambafu zake
 
Back
Top Bottom