Naombeni ushauri wakuu

Anko Kong

Senior Member
Joined
Jul 3, 2020
Posts
130
Reaction score
72
Mmeshindaje wakuu

Nimeanzisha ujenzi wa nyumba tangu mwaka Jana nyumba imeishia kwenye lenta pesa zikaniishia.

Sasa nimejichanga nimepata milion 4 nawaza sijuwi nimalizie nyumba yangu halafu niizeke maana mkoani kwetu ujenzi ni gharama nafuu kidogo au nifanye biashara ili niweze kuizalisha ili baadae nimalizie nyumba yangu, sina biashara yeyote kwa sasa naombeni ushauri wenu wakuu.
 
Malizia nyumba yako kwanza

Biashara hizi ni bahati nasibu.

Utatafuta mtaji wakati mwingine.
 
Tumia hiyo 4 millions kumalizia nyumba yako na kisha endelea na kile kilicho kufanya ukaipata hiyo 4 millions ili upate mtaji.
 
Tumia hiyo 4 millions kumalizia nyumba yako na kisha endelea na kile kilicho kufanya ukaipata hiyo 4 millions ili upate mtaji.
Nilikuwa na kaz mkataba wake umemalzka
 
Nilikuwa na kaz mkataba wake umemalzka
Okay....
Kama nyumba imepanda hadi kwenye lenta, basi nyenyua hanam kwa kiasi cha vyumba viwili, kisha paua hivyo vyumba kwa mtindo wa sloop, weka mlango mmoja wa grill ambao utaweza kucover hivyo vumba mbili na madirisha mbili, na hakikisha unatumia pesa isiyo zidi 2 millions.

Baada ya hapo hiyo 2 millions inayo baki hakikisha unaanza biashara ndogo kwa nusu ya pesa ulionayo (1,000,000) na tunza nusu (1,000,000) for emergency.
 
Kwamfano:-

1. Kumalizia hanam ya room mbili kwa mtindo wa sloop itahitaji tofali sio zaidi ya 150 ambazo zitagharimu 150,000.

2. Kuzijenga tofali 150 itahitaji comment mifuko 2 ambayo itagharimu 30,000.

3. Lori 2 za mchanga ambao utajengea hanam na kupiga ripu pamoja na sakafu 200,000.

4. Madirisha mbili na mlango moja wa grill itakugharibu 400,000

5. Cement miko 7 ambazo zitatosha kupiga ripu na sakafu za chumba mbili, zitagharimu 100,000.

6. Mbao kwaajili ya kecho ya bati la slopu pamija na misumari itakugharimu 200,000.

7. Bati 24 za futi sita kilamoja, zitagharimu walau 400,000

8. Ufundi na mengineyo kadiria 500,000

Jumla ya pesa itakuwa umetumia ni walau shilingi 1,980,000
 
Asante kwa ushauri wako mkuu
 
Nmekuelewa mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…