Naombeni ushauri wana jf

Naombeni ushauri wana jf

AMOURY

Member
Joined
Aug 17, 2009
Posts
6
Reaction score
0
Ni matumaini yangu kuwa mu wazima!
Ni hivi mi nina tatizo la kifua linanisumbua kwa muda sasa.

kifua kinauma kwa ndani upande wa kulia hii hutokea nikiwa nataka kuamka kama nimelala au nimekaa kwenye sofa, hasa nikiwa sehem za baridi.

nimeenda hospitali (muhimbili) nikapiga x- rays haujaonekana ugonjwa wowote,zaidi niliambiwa kuwa nina alregic chest, haya majibu niliwahi kupewa pia nilipoenda kupima hospitali moja iko mwenge.

Nilipokuwa morogoro nako nilipiga x-rays hawakuona ugonjwa pia.
Swali langu ni hili.

kama ugonjwa hauonekani sasa naumwa kitu gani. na hiyo alregic chest haina dawa maana wao(doctors) wananipa antibiotic nikameze ambazo nazo hazijanisaidia.
Nawasilisha
 
Tuweke pembeni utani, matatizo yote haya ambayo hospitali yanashindikana, basi wahi Loliondo!...!100% utapona!
 
Tuweke pembeni utani, matatizo yote haya ambayo hospitali yanashindikana, basi wahi Loliondo!...!100% utapona![/QU
Babu wa loliondo anatibu ukimwi,kisukari,pumu,na shinikizo la damu. sasa huyu jamaa anumwa kifua. namshauri akacheki hospitali zenye vipimo vya uhakika.
 
Jitahidi kutokuacha kifua wazi hasa unapokuwa sehemu za baridi. Itakusaidia, hakikisha ukilala uvae hata tshirt ili tu usiache kifua kikapigwa baridi.
 
Back
Top Bottom