Akiondoka anaondoka na watoto Pia au Ananondoka Mwenyewe? Una Uhakika hao watoto ni wakwako au wa huyo wa Moshi.. Je Kikifika Kipindi cha kubeba ujauzito wa hao watoto wawili alikuwa akienda Pia kwao?
Najaribu kuwaza Maake hizi safari za Mke kwenda kwao hazijawahi kuiacha ndoa Salama hasa pale wazazi wa Mke ndio wako Nyuma na Baraka Tele wametoa.
Ogopa Sana mzazi kumkaribisha Mtoto wake wa Kike kukaa kwao hata zaidi ya Wiki bila kuambatana na Mume wake..
Labda tena nikuulize Mumefunga Ndoa au mlijikuta tu Mko wote Pamoja. Kama hamjawahi kufunga Ndoa aisee na kama umekuwa ukitoa ahadi usizozitimiza basi Kazi ndio Imeanza.
Nachangia Tu wala sina nia Mbaya.