Naombeni ushauri wenu jamani kwenye hii biashara ya kusaga mahindi

Naombeni ushauri wenu jamani kwenye hii biashara ya kusaga mahindi

Inataka mtaji mkubwa vinginevyo uwe na mbinu za au watu wa kushirikiana nao ingawa mbinu hii inakufanya uone faida kuwa ndogo kwakuwa itagawanyika zaidi.
 
Habari yenu wakuu,

Mimi ni kijana wa kiume nina umri wa miaka 29, elimu yangu ni shahada ya kwanza.

Ni hivi baada ya kuhangaika kwa muda mrefu kutafuta kazi bila mafanikio yoyote, hivi karibuni nimekutana na jamaa mmoja, yeye ni muajiriwa serikalini na anataka kuanzisha biashara yake ya kusaga mahindi, kupack unga na kusambaza kwa wateja.

Sasa huyu jamaa changamoto aliyokua nayo ni kwamba hana muda wa kutosha kusimamia biashara atakayoianzisha, hivo kutokana na mimi sina kazi hivi sasa, ameniomba niwe msimamizi wa biashara yake na faida itakayopatikana atanipatia asilimia 30.

Na huyu jamaa anataka kununua mashine zake mwenyewe za kusaga mahindi.

Hivyo naombeni ushauri wenu jamani wazoefu wa hii biashara au wenye uelewa wa hii biashara katika mambo yafuatayo,

1.)Upatikanaji wa malighafi yaani mahindi mazuri.

2.) Soko lake lipoje?

3.) Upatikanaji wa vifungashio upoje?

4.) Ushindani katika soko upoje?

5.) Utaratibu wa kufanya hii biashara kisheria upoje? namaanisha utaratibu wa kusajili na kupata vibali katoka mamlaka husika.

6.) Kodi ipoje?

7.) Upatikanaji wa mashine na gharama zake zipoje?

8.) Ipi sehemu nzuri ya kufanyia hii biashara? Jamaa na mimi tupo DSM

9.) Changamoto ya hii biashara ipoje?

10.) Wapi yanapatikana mahindi mazuri?

11.) Vipi kuhusu usimamizi wake upoje?

12.) Changamoto zake zipoje?

13.) Faida yake ipoje?


Ni hayo tu ndugu zangu, naombeni msaada wenu kuyajua ili niweze kuilewa hii biashara angalau nipate pa kuanzia kama msimamizi.

Ahsanteni sana!









Sent using Jamii Forums mobile app
Nilichojifunza katika biashara ni kutokufanya hesabu kabla ya kuanza.
Hesabu zitakupoteza na kukukatisha tamaa. Ndiyo maana wafanyabiashara wengi hawajui kitu kinaitwa RISK analysis. Yeye akiona fursa anayo na anatusua
 
Back
Top Bottom