Naombeni ushauri wenu wa busara

Nyalotsi

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2011
Posts
6,986
Reaction score
5,058
Nina mchumba wangu tunaishi sehemu tofauti tena mbali. Kuna tabia anaifanya sivutiwi nayo. Hii tabia ni ya kunibeep, kutuma tafadhali nipigie au naomba niongeze salio. Hii imekuwa ikijitokeza mara nyingi mpaka nafikia kukereka moyoni. Huwa nampigia mara nyingi kwa siku tunaongea na huwa namwongezea salio pale ninapokuwa nazo. Lakini mwenzangu muda wowote atatuma tafadhali nipigie au naomba niongeze salio. Kwa kweli nachukizwa na hii tabia ila kumwambia naona kama ataudhika na kuanza kutofautiana. Nampenda sana na nimeshamtambulisha home. Huko nyuma kuna binti niliwahi kuachana naye sababu ya mambo haya. Ulikuwa ukimtumia salio hakupigii ila anakubeep na kutuma tafadhali nipigie,nilimwelimisha lakini hakubadilika. Nikahisi ni utoto hivyo bora nimuache na watoto wenzie(alikuwa first yr chuo). Sasa huyu ni mfanyakazi bado ni yale yale. Hivi wadada wote mko hivi? Nitafanyaje ili nimfikishie ujumbe bila kuvuruga uhusiano wetu? Nampenda sana,nahisi hii kitu itatuvuruga.
 
Jide alishawah kuimba kitu cha "wanaume kama mabinti".
 
Nipe namba yako nikupunguzie salio wewe na mpenzi wako.
 
Jambo la kwanza ambalo mimi ningekushauri ufanye ni kuvunja ukimya na kuongea na mwenzi wako juu ya swala hili. Mweleze ni jinsi gani unakereka na jambo hili na namna ambavyo ungependa awe, kama kweli anakupenda atakusikiliza na atabadilika na kama asipobadilika basi ujue huyo hakufai. She is not your type.
 

asante mkuu,lakini sina uhakika atalipokeaje hili jambo. Naomba wadada waongee,wangejisikiaje kuambiwa hivyo. Maana yule wa kwanza nilipomweleza akawa anadai simpendi na nimepata wengine.
 
Ndiyo tabia za hivi viumbe. Kubebwabebwa tu. Hata mawaziri wanawake ndiyo zao hizo kwa wanaume wao. Huna jinsi mvumilie tu.
 
usipoziba ufa utajenga ukuta,navojua mimi mapenzi nimawasiliano ikiwa nipamoja nakuambizana ukweli hatakama unuma mwambie unavojickia nayeye anatakiwa akuelewe vingnevyo mbele yasafari utashindwa kukemea makosa mengne makubwa kisa unaogopa atachukia.
 
Mimi ni mwanamke kwa upande wangu kabla hatujaoana sikupenda kabisa hy mambo ambayo mchumba wako anakufanyia! Ina maana yeye huwa anampigia nani km unampa vocha na bado anakubip? Wanawake wa staili hii ni hatari sn, hata mliwa kwenye ndoa, usitegeemee mshahara wake kusaidi mahitaji hom, utawajibika kwa kila kitu. Utakuta hata ukipanda daladala hawezi lipa npk we ulipe. Mchumba anayefaa hawezi kuluchuna vocha kihivyo kwanza huwa ana uchungu na pesa yako. Kaa chonjo utaishia kuhonga usipokuwa makini!
 
haya mambo ya simu za mkononi yame-complicate sana maisha...; mahusiano yanavunjika, watu wanakufa, yaani balaa tupu
 

Hili nalo NENO.
 
nyalotsi,
kuna baadhi ya tabia za wenza wetu, kama ulishaongea nae ukaona habadiliki ina maana ndivyo alivyo hawezi kubadilika at per, itachukua muda.... na kama tabia hiyo haikuletei madhara yoyote si umkubali jinsi alivyo? mapenzi si rahisi kama wengi wanavyodhani kuna baadhi ya vitu unakubali na kuona vya kawaida, as long as haikuchubui wala kukudhuru......

afterall utaacha wangapi? maana wanawake wengi wana tabia hiyo..... unless humtaki
 
haya mambo ya simu za mkononi yame-complicate sana maisha...; mahusiano yanavunjika, watu wanakufa, yaani balaa tupu

yaani,natamani hata simu zisingekuwepo! Somtime naweza kufikiria sijui nizime simu niwe nawasha wikend tu! Kwa namna inavyokwenda nahisi option ntakayochukua italeta shida upande mmoja ikasababisha mahusiano yetu kuwa compromised.
 
BT ndo maana naomba ushauri maana aliyepita nilimwacha kwa sababu hiyo. Ndo maana nikauliza hivi hii ndo tabia ya dada zetu? Hata kama una kazi yako.? Kwa kweli nachukia kutumiwa tafadhali nipigie,inakuwa kama emergence fulani wakati ni maongezi ya kawaida ambayo ni kawaida kuongea naye. Asante kwa ushauri!
 
Muulize hizo vocha huwa anapeleka wapi mpk kila siku anaishia kukubip na kutuma plz col me. Ukiona hupigiwi weye anapigiwa mwngne yakheee!!
 
usipoziba ufa utajenga ukuta,navojua mimi mapenzi nimawasiliano ikiwa nipamoja nakuambizana ukweli hatakama unuma mwambie unavojickia nayeye anatakiwa akuelewe vingnevyo mbele yasafari utashindwa kukemea makosa mengne makubwa kisa unaogopa atachukia.

kuna mambo nilishamwambia siyapendi na huwa hayafanyi. Ila kwa hili la mawasiliano sijajua wenzetu huwa wanachukuliaje.! Nikimwambia usinibeep au kunitumia tafadhali nipigie atareact vipi? Au ndo ataanza kutafuta mtu wa kubadili? Au atakubaliana na mimi? Hapa nimestuck kwa kweli!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…