Nyalotsi
JF-Expert Member
- Jul 20, 2011
- 6,986
- 5,058
Nina mchumba wangu tunaishi sehemu tofauti tena mbali. Kuna tabia anaifanya sivutiwi nayo. Hii tabia ni ya kunibeep, kutuma tafadhali nipigie au naomba niongeze salio. Hii imekuwa ikijitokeza mara nyingi mpaka nafikia kukereka moyoni. Huwa nampigia mara nyingi kwa siku tunaongea na huwa namwongezea salio pale ninapokuwa nazo. Lakini mwenzangu muda wowote atatuma tafadhali nipigie au naomba niongeze salio. Kwa kweli nachukizwa na hii tabia ila kumwambia naona kama ataudhika na kuanza kutofautiana. Nampenda sana na nimeshamtambulisha home. Huko nyuma kuna binti niliwahi kuachana naye sababu ya mambo haya. Ulikuwa ukimtumia salio hakupigii ila anakubeep na kutuma tafadhali nipigie,nilimwelimisha lakini hakubadilika. Nikahisi ni utoto hivyo bora nimuache na watoto wenzie(alikuwa first yr chuo). Sasa huyu ni mfanyakazi bado ni yale yale. Hivi wadada wote mko hivi? Nitafanyaje ili nimfikishie ujumbe bila kuvuruga uhusiano wetu? Nampenda sana,nahisi hii kitu itatuvuruga.