Naombeni ushauri wenu

smtext

Member
Joined
Nov 1, 2013
Posts
10
Reaction score
1
mimi ni kijana wa kiume umri ni miaka 22.ninaishi na mama yangu kwani baba alitangulia mbele ya HAKI miaka mingi iliyopita pindi nikiwa darasa la tatu.Nimeishi na mama yangu kwa muda wote na nimefanikiwa kufika kidato cha sita nilipokuwa nikisoma masomo ya PCB na kuhitimu mwaka 2012.matokea yangu hayakuweza kuniwezesha kwenda chuo kikuu kwani nilipata E,S,S. mwaka mmoja baada ya kuhitimu kidato cha sita niliomba nafasi wizara ya afya na nimefanikiwa kuchaguliwa kusoma "clinical medicine" katika moja ya vyuo vya serikali{wizara}.muda wa kwenda shule umefika TATIZO ada imekuwa shida maana mama yangu ambaye ninamtegemea kwa kila kitu ni MGONJWA na hawezi kumudu gharama za ADA YA CHUO.naombeni ushauri nifanye nini??
 
muda wa kwenda shule umefika TATIZO ada imekuwa shida maana mama yangu ambaye ninamtegemea kwa kila kitu ni MGONJWA na hawezi kumudu gharama za ADA YA CHUO.naombeni ushauri nifanye nini??
  • Pole sana.
  • Nenda kalipoti chuo husika mapema.
  • Angalia katika joining instruction, kuna michango kidogo ya usajili ambayo ni lazima utoe kwa mwanachuo mpya, tafuta hiyo fedha ya usajili kwanza.
  • Baada ya kupata usajili na kutambuliwa kuwa wewe ni mwanachuo, fuata taratibu za kuonana na uongozi wa chuo kwa msaada zaidi wa ushauri na nini kifanyike ili kupata msaada ili kuendelea na masomo yako.
  • ​Hakika utafanikiwa, usirudi nyuma.
 
duuh! pole ndugu yangu,fanya usajili kwanza halafu mambo mengine yatafuata,vilevile mshirikishe MUNGU atafanya njia pasipo na njia.
 
Mungu ni muweza wa yote, fanya maombi ya kufunga omba sana na Mungu atafungua milango,soma Yeremia 33.3, Yeremia 29.11, hakuna jambo linaloshindikana kwake Mungu, atakusaidia tu mdogo wangu. Pia waweza kwenda sehemu ya ibada unakoabudu mwambie kiongozi wako kama ni Mchungaji, Padre au Shekhe, atakutangaza pale uapoabudia wapo watu wenye mioyo ya huruma, upendo na utoaji watakusaidia, pole ila Mungu yupo pamoja na wewe na utafaulu na siku moja utakuwa kazini ukipokea mshahara wako, hayo ni majaribu tu, yatapita, pia sikiliza wimbo wa Upendo Kilahiro usemao " HILO NALO LITAPITA"
 
nashukuru ndugu zangu kwa ushauri mnaoendelea kunipa maana unatia matumaini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…