mimi ni kijana wa kiume umri ni miaka 22.ninaishi na mama yangu kwani baba alitangulia mbele ya HAKI miaka mingi iliyopita pindi nikiwa darasa la tatu.Nimeishi na mama yangu kwa muda wote na nimefanikiwa kufika kidato cha sita nilipokuwa nikisoma masomo ya PCB na kuhitimu mwaka 2012.matokea yangu hayakuweza kuniwezesha kwenda chuo kikuu kwani nilipata E,S,S. mwaka mmoja baada ya kuhitimu kidato cha sita niliomba nafasi wizara ya afya na nimefanikiwa kuchaguliwa kusoma "clinical medicine" katika moja ya vyuo vya serikali{wizara}.muda wa kwenda shule umefika TATIZO ada imekuwa shida maana mama yangu ambaye ninamtegemea kwa kila kitu ni MGONJWA na hawezi kumudu gharama za ADA YA CHUO.naombeni ushauri nifanye nini??