Naombeni ushauri

Naombeni ushauri

strawberry1

Member
Joined
May 7, 2011
Posts
35
Reaction score
6
Nina Tshs 1,000,000/= nataka kuanzisha biashara. Ninazo idea mbili tofauti kichwani:-
1. Nifungue duka la vitu vya nyumbani kmf. chumvi, sabuni, unga, mchelle, mafuta n.k
2. Nifungue Genge

Naomba ushauri ni biashara gani itakuwa feasible kwa hicho kianzio?
 
kwanza kabisa amua eneo la kufanyia biashara, pili angalia kama kuna kodi zozote unahitajika kulipa. kisha angalia umebaki na pesa ngapi. kama pesa iko chini ya laki 6. anzisha genge pesa iliyobaki kaifungulie Fixed account. Pili, kama hujawahi kufanya biashara kabisa, nakushauri anza na genge ili uone TAMU na CHUNGU ya biashara. Pesa iliyobaki weka fixed. Kwa nini fixed? kwa sababu itakuwa mbali na wewe kiasi kwamba unapoanza kupata hasara usiifikirie kuichukua. Kumbuka kila biashara huanza na hasara kwa muda ndipo itoe faida kamili
 
Back
Top Bottom