Unaona maovu ya huyo baba mtoto kwa kuwa unaishi nae? Are you sure kwamba huyo ex hadanganyi? Are you sure kuwa huyo ex atakuoa kweli? Fimbo ya mbali haiui nyoka, ushikwapo shikamana, bora moja shika kuliko kumi nenda uje, Zimwi likujualo halikuli likakwisha, ukipata kipya usitupe cha zamani, mla mla leo mla jana kala nini... ni baadhi tu ya misemo ambayo inakutahadharisha kabla hujachukua uamuzi wa kumuacha uliye nae kwa sasa, ukaenda kwa 'rehani'... Kama kuna sehemu unaweza kwenda kukaa (kwa wazazi au ndugu au rafiki), kwa ujanja wote wa kike muage huyo uliye nae kwa sasa kama unaenda kusalimia, kaa mbali nae kwa japo mwezi mmoja, then jaribu kuusikiliza moyo wako, na pata muda huru zaidi wa kumsoma tena huyo ex. Najua kwa sasa mnakutana kwa siri na huyo ex- lakini inawezekana na wivu tu unamsababisha akuhadae uachane na uliye nae, lakini pengine ukishaachana nae, atakutosa au naye ataanza vituko. So, jaribu kuondoka (kwa amani) kwa huyo uliye nae, wakati huo huo mdanganye huyo wa zamani kuwa ndo ushaachana na huyo baba mtoto, then msome kama atakuwa responsible na kuendelea na nia yake ya ndoa, lakini pia tumia huo mda kusoma tabia zake...