Mkuu, anza kwa kupata kibali cha Serikali ya Mtaa/Kijiji na Kata, kisha wasilisha wazo kwa Halmashauri ili kujua taratibu za eneo na vibali vinavyohitajika. Pia tafuta eneo linalofaa, tengeneza utaratibu wa wafanyabiashara kulipia nafasi, usafi na ulinzi. Muhimu zaidi, anza kwa gulio la majaribio mara 1 kwa wiki uone mwitikio kabla ya kulifanya rasmi.Nawasalimu nyote.
Nipo Kwa majumu ya kikazi katika kata flani ambayo ina wakazi wengi na imechangamka kwa kiasi cha kuridhisha.
Changamoto nikwamba kata hii haina gulio au soko ambalo wakazi wahapa wanaweza kupata bidhaa ndogo ndogo ambazo kwa kawaida hupatikana magulioni. Ili kupata mahitaji muhimu inawalazimu kusafiri umbali wa kilometa25-35 kwenda wilayani ambapo kuna gulio la mara moja kwa wiki.
Nimejaribu kuongea na wakazi wengi wa eneo hili na asilimia kubwa wabatamani uwepo wa huduma ya gulio katika eneo hili.
Swali langu kwenu , nihatua gani zakufuata ili kuanzisha gulio la angalau mara moja kwa wiki?
Asante mkuuMkuu, anza kwa kupata kibali cha Serikali ya Mtaa/Kijiji na Kata, kisha wasilisha wazo kwa Halmashauri ili kujua taratibu za eneo na vibali vinavyohitajika. Pia tafuta eneo linalofaa, tengeneza utaratibu wa wafanyabiashara kulipia nafasi, usafi na ulinzi. Muhimu zaidi, anza kwa gulio la majaribio mara 1 kwa wiki uone mwitikio kabla ya kulifanya rasmi.
Asante kiongoziHuna haja ya kutafuta kibali kutoka sehemu yoyote. Kama utaweza tafuta speaker zako zile za kuchaji ili uweze kutangaza na kuwaburudisha wateja wako na nyimbo za hapa na pale.
Pili uwe ushafanya utafiti wa mahaitaji yao ya bidhaa na uchague siku moja kati ya jumapili au jumamosi kwa ajili ya huo mnada wako.
Ukishachagua siku basi hakikisha unakuwa na muendelezo hadi wanakijiji waawe wanajua siku fulani nitapata mahitaji yangu sehemu fulani.
Baada ya hapo unaweza kuwa unapita kutangaza kijijini kwamba mnada utakuwepo kama kawaida na offer kabambe zitakuwepo.
Hadi kufikia hapo bila shaka kuna wazee wa fursa watakuwa wamejiunga nawe. Na ndio hapo mtaijulisha serikali ya mtaa sasa na ndio ianze kukusanya ushuru.
Asante mkuu. Namimi nia yangu haikuwa kuanzisha gulio langu ila nilitaka mchakato wakufuata ili wakazi wahapa tulifatilieNenda ofisi ya kata au kijiji ushauriane na viongozi ili muanzishe, hayo magulio yanaanzishwa na kuendeshwa na ofisi ya mkurugenzi wa halmashauri kupitia ofisi ya mtendaji kata au kijiji katika eneo husika, mtu binafsi huwezi kumiliki gulio lako