Jaman, kwanza nawasalimu kwa jina la mungu, na natumai ni wazima wa afya ila kama afya iko vibaya mungu akupe ahueni🙏
Wakuu mim ni mwanachuo naesoma Bachelor of education in science (physics).
Naombeni maoni yenu kama wakubwa zangu wenye upeo mkubwa juu ya hii kozi yangu kama mnavojua changamoto za ajira, mishahara na mengineo.
Nakalibisha mjadala, naomba tuchangie maoni yoyote.
Mungu awape mchana mwema🙏🙏
Upo mwaka wa ngspi?
Siku wanapunjwa mishahara sana sawa na wa art ktk sekta binafsi.
Physics ni broad subject so kuwa makini. Unaweza maliza ukawa mediocre graduate bila kujali A na B ulizopata.
Ushauri wangu :
Jikite ktk technical skills japo department ya Fizikia(udsm) haina kama hawajabadili mtaala.Ssa wewe ufanya option( very important).
Fanya option ya
- graphics design
-computer maintainance and installation
-Introduction to computer science
-computer programming
-computer programming kamac/java ++ na python,html,css na javascript.
-data base evelpment au maintanance
-digital circuits ipo department ya IS
-Electronic science(huwa hawaimalizi hii kozi, wewe ongeza mpaka microprocessor na microcontroler, device troubleshooting nk) hii itakusaidia ukiamua kujiongeza kufanya electronics devices troubleshooting and system design kama simu na tv, nk.
-Electromagnetism, hii topic ina kila uchafu wa kila kitu kilichoundwa na binadamu, kuanzia simu,computer. Motor nk. Ni msingi wa teknolojia ya vitu vyote vya umeme. Nimejikita zaidi iwapo utakosa ajira za mashuleni na vyuoni.
Mtaala wa fizikia huwa wa kiduwanzi haukupi tecnical skills za ulimwengu wa sasa labda kama kuna mabadiriko.