Naona Anguko la SIM Pesa

Naona Anguko la SIM Pesa

Kasomi

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2014
Posts
11,030
Reaction score
20,391
Habari wakuu bila shaka leo ndio tarehe yenyewe yaani mabadiliko ya miamala kwenye mifuko ya simu yameanza kutumika.
Bila shaka kila mtu ambaye anafanya miamala kwenye simu amekumbwa na hilo pia najua limewasikitisha na hapo ndo maana halisi ya neno la Rais Samia kwamba wampe mda ajenge kwanza uchumi

Mitandao ya simu inaenda kupata pigo au Anguko la miamala kwa mitandao yote kwa sababu ongezeko la makato litawafanya watumiaji wengi wa simu kwa ajili ya miamala kuanza kutumia Benki.
Pia ongezeko hili ni pigo tosha kwa wananchi hasa na wale ambao wanakaa maeneo ambayo mabenki yenye Makao nafuu hayapatikani.

Mabadiliko ya miamala yaliyo fanyika ni kama ifuatavyo

GHARAMA ZA KUTOA NA KUTUMA PESA KWA NJIA YA SIMU KUANZIA LEO TAREHE 15/07/2021

•Kutoa 100,000 ilikua 3600 sasa hivi 6,100
•Kutoa 200,000 ilikua 5,300 sasa hivi 8,240
•Kutoa 300,000 ilikua 6,500 sasa hivi 10,000
•Kutoa 400,000 ilikua 7,000 sasa hivi 11,100
•Kutoa 500,000 ilikua 7,500 sasa hivi 12,700
•Kutoa 600,000 ilikua 8,000 sasa hivi 13,900
•Kutoa 700,000 ilikua 8,000 sasa hivi 15,100
•Kutoa 800,000 ilikua 8,000 sasa hivi 15,520
•Kutoa 900,000 ilikua 8,000 sasa hivi 16,900
•Kutoa 1,000,000 ilikua 8,000 sasa hivi 17,400
•Kutoa 3,000,000 ilikua 10,000 sasa hivi 20,000


List hii inaonyesha Makato ya Zamani na Makato yatakavyokua kuanzia leo tarehe 15/07/2021


Mimi kama mzalendo mpya nasema kwamba mifumo ya utawala wa
CCM
ni takataka mnabisha haya twendeni sasa.

Najua mtashangaa kwamba nimeanza kuiponda CCM lini lakini ndio hivyo mimi ni mzalendo mpya.
Tupende nchi yetu.
 
Mpendwa ATM kadi,
Nachukua nafasi hii kukuomba msamaha kwa jinsi ambavyo nilikutenga, sikukujali wala kukuona wa maana!! Hakika nimeamini wewe ni rafiki wa kweli. Tusahau yalopita, tugange yajayo.
Wako mtiifu/Pendoni
MERCIFUL
 
Mpendwa ATM kadi,
Nachukua nafasi hii kukuomba msamaha kwa jinsi ambavyo nilikutenga, sikukujali wala kukuona wa maana!! Hakika nimeamini wewe ni rafiki wa kweli. Tusahau yalopita, tugange yajayo.
Wako mtiifu/Pendoni
MERCIFUL
Kweli kabisa muombe msamaha ATM maana ulimtenga na sasa unaenda kumtumia zaidi
 
IMG_0890.jpg

Nishachangia kodi ya serikali ntafanyaje sasa

Ila inaumaa
 
Back
Top Bottom