Naona Bunge linapiga chafya

Naona Bunge linapiga chafya

Kwa kweli pasipo kupoteza muda, ninayo furaha ya dhati toka moyoni kwa hiki ambacho nimekiona kwa bunge la leo!

Yaani ni kama mgonjwa mahututi ambaye ghafla ameanza kupiga chafya!

Chafya ni dalili ya uhai.

Hongereni sana wabunge wote mliohusika kukemea vibaka walioko kwenye wizara mbalimbali ambao kazi yao ni kuiba na kuiba na kuiba tena!

Rais Samia Suluhu Hassan aliwaambia wajitathmini, lakini hadi sasa hatujaona mtendaji yeyote serikalini akijihudhuru au hata kuomba radhi tu kwa kile kilichotokea!

Wabunge naomba msiishie tu kutufurahisha wananchi wenu kwa maneno mazito mazito mnayoyasema huko, bali hakikisheni wahalifu wote wanachukuliwa hatua ili kuinusuru nchi yetu na hawa mchwa wanaokula kila kitu hadi vyuma wao wanakula tu!
Ccm ni ileile tu wacha kudanganywa ndugu
 
Kwa leo angalau wabunge wa sisiyemu wameonesha uhai wao kwa kuikemea mijizi iliyo serikali kuu na mamlaka za serikali za mitaa ambayo imetafuna mabilioni ya fedha za wavuja jasho pasipo aibu.Hebu nendeni mbele zaidi kwa kuishauri serikali liwe jua au mvua hao wezi waende wakanyoe
Wenyewe ni majizi
 
Hilo bunge ni furahisha genge, kama kweli wanajiamini wafanye azimio la bunge kuwatoa baadhi ya mawaziri. Kinyume na hapo ni maigizo kama kawaida.
Upo sahihi kabisa
 
Kwa kweli pasipo kupoteza muda, ninayo furaha ya dhati toka moyoni kwa hiki ambacho nimekiona kwa bunge la leo!

Yaani ni kama mgonjwa mahututi ambaye ghafla ameanza kupiga chafya!

Chafya ni dalili ya uhai.

Hongereni sana wabunge wote mliohusika kukemea vibaka walioko kwenye wizara mbalimbali ambao kazi yao ni kuiba na kuiba na kuiba tena!

Rais Samia Suluhu Hassan aliwaambia wajitathmini, lakini hadi sasa hatujaona mtendaji yeyote serikalini akijihudhuru au hata kuomba radhi tu kwa kile kilichotokea!

Wabunge naomba msiishie tu kutufurahisha wananchi wenu kwa maneno mazito mazito mnayoyasema huko, bali hakikisheni wahalifu wote wanachukuliwa hatua ili kuinusuru nchi yetu na hawa mchwa wanaokula kila kitu hadi vyuma wao wanakula tu!
Wewe na wabunge wenu wote wapuuzi tu. Pesa yenu tutaila sana na hakuna wa kutufanya lolote.
 
Kama anapiga chafya... angalia kwenye paji la uso hakuna vijasho vidogo vidogo...? Kama vipo tuandae matanga hiyo sio dalili nzuri Kwa mgonjwa...😭😭😭​
 
Nimemuona Madelu amechanganyiikiwa
Yaani ni aibu kubwa sana kwa hawa watu
Halafu mwizi utaona anavyobabaika
Wabunge lazima watunge sheria sio tu uchaguzi ukikaribia ndio wanaanza kuangalia watakula nini miaka mitano mingine

Hizi kelele zitaisha wala hawatafanya kitu kwani wote wanajuana wanakula sahani moja
 
Kwa leo angalau wabunge wa sisiyemu wameonesha uhai wao kwa kuikemea mijizi iliyo serikali kuu na mamlaka za serikali za mitaa ambayo imetafuna mabilioni ya fedha za wavuja jasho pasipo aibu.Hebu nendeni mbele zaidi kwa kuishauri serikali liwe jua au mvua hao wezi waende wakanyoe
Kukemea hakuondoi ufisadi wala hauwatishi mafisadi,wizi uko palepale
 
Back
Top Bottom