Kila nikijaribu kukata tamaa naona sura ya Fiston Mayele ikitabasamu ndani ya stage ya Al-hilal Sijui ina maana gani
Shida yenu yanga mnajiangalia nyie tu, hamuangalii strength ya mpinzani au labda hamuwajui vizuri Al Hilal.
Wale jamaa wamewazidi vitu vingi kuanzia pesa waliyonayo, uwekezaji mkubwa waliofanya na hata wachezaji wao ni wazuri mara 2 ya kwenu.
Unapomtaja Mayele wenzako wana Mohamed Abdel Rahaman uyo jamaa ni hatari.
Ukimtaja Morrison ambae hajui hata kufunga wenzako wana Makabi Lilepo.
Ukimtaja Kisinda na Moloko ambao wanakimbia pasipo malengo na hawajui kufunga wenzako wana Lamine Diadhiou msenegali aliesajiliwa kwa bilioni 1.
Mabeki wenu hawafikii uwezo wa beki tatu Ibrahim Moro na Vidinho alietoka Petro Atletico iliofika nusu fainali msimu uliopita.
Ogopa sana kucheza na timu yenye malengo ya kufika fainali wakati ninyi malengo yenu ni kufika makundi hapo hata effort mtatofautiana. Walivyocheza Hilal hapa sivyo watakavyocheza kwao. Approach ya ugenini na nyumbani haiwez kufanana ndo maana Al Ahly ya Misri wakija hapa unaweza dhani ni Ihefu.
Kwaiyo msijidanganye nyie Uto, kama hamjui atmosphere ya uwanjani kwao pale nendeni mkamuulize Iddriss Mbombo ameshacheza pale misimu miwili atawaambia.