naona kama biashara ya kutafsiri vitabu kwa kiswahili inaweza kulipa.

Red Giant

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2012
Posts
15,657
Reaction score
20,967
Nimekuwa nawaza kuwa biashara kama hii inaweza kulipa. Ukiangalia kuna vitabu vimeuza sana duniani. Kuna vitabu kama think and grow rich cha Napoleon hill kimeuza nakala 70m, the hobbit 100m, series ya harry potter imeuza 450m na the 7 habits of highly effective people 25m. rich daddy poor daddy kimeuza nakala 26m.


Naamini ukivitafsiri kwa Kiswahili hivi vitabu na ukavitangaza hauwezi shindwa uza nakala 10,000-20,000. Nafikiri vitu muhimu ni kuelewana na wenye hati miliki, kupata watafsiri na namna ya ya uchapishaji.


Uchapishaji wa vitabu ni gharama ndogo sana. Mwaka juzi nilichapa kitabu cha page 60, paperback , karatasi nyeupe na lamination ya nylon kwa 1,200 kwa kitabu. Waliniambia siku nikitaka batch nyingine watanipunguzia labda kufika 900. Hii inamaana kitabu kama gifted hand chenye page 224 unaweza chapisha kwa 3,600. Hiki kitabu amazon kinauzwa dola 6 ambazo ni sawa na sh 10,500 mitaani wengi wanauza 15,000.

Challenge kubwa ya hii biashara ni usambazaji na kuitangaza.
 
Yote yanawezekana fuata copyright policy

Mkuu hii ni biashara tumia fursa ulioina ni lazima utoke mkuu, chamuhimu ni kuvitangaza, mwanzo kidogo utakuwa mgumu ila watu wakikuelewa unatoka, shida watakuja watu wengi kuvamia biashara hii ikishashika hatamu.
 
mkuu hii biashara inawezekana na italipa sababu kiswahili kwa sasa kinatumika katika ukanda wote huu,cha msingi ni copyright tu na matangazo.
 

Mkuu ni idea nzuri. Ila there is a wark=ning. Watanzania hatuna tabia ya kusoma vitu hasa vile vinavyonoa ubongo. Labda kwenye marking stretegy yako uweke na uhamasishaji wa usomaji vitabu
 
Mkuu ni idea nzuri. Ila there is a wark=ning. Watanzania hatuna tabia ya kusoma vitu hasa vile vinavyonoa ubongo. Labda kwenye marking stretegy yako uweke na uhamasishaji wa usomaji vitabu
kwa kuanza inabidi kuangalia ni vitabu gani vinapendwa sana. vitabu kama Think big, rich daddy poor daddy, mossad, the 7 habits of highly effective people na baadhi vya hadithi watanzania wanavipenda sana. kiufupi wengi wanapenda vitabu vya self help.
 
LAbda mkuu ungefanya ka survey kidogo kujua target customers ni wapi. Watatnzania kama watanzania ni wengi sana na wanatofautina. KWa hiyo ukijua hao customers elfu kumi watatoka kundi gani then itakuwa rahisi hata kwenye uandikaji wa business plan yako. Mimi binafsi napenda hivyo vitabu. KAma upo very serious mkuu tuongee. We can even think of kindle readers amabzo zitawawezesha watu kununua vitabu vingi kwa bei nafuu. Tuongee private mkuu kama upo tayari tayari
 
bahati mbaya sasa kuna vitu vimenipin down. ila nilikuwa natoa tu idea. tafuta mtu aliye tayari mpige kazi. humu wako wengi sana.
 

hili ni wazo zuri. tatizo ni jinsi gani utawadhibiti "infringers" ambao watasubiri nakala zako ziingie mtaani kisha wao
wananakili na kuziingiza mtaani kwa bei poa kuliko zako!

kwa bongo ufuatiliaji wa haki miliki ni hafifu sana. hata huko kwenye muziki ambako watu wameamka kiasi unakuta nakala feki kibao mtaani. ukija kwenye vitabu ukiingia hata baadhi ya maduka ya vitabu ukiangalia baadhi ya vitabu ni feki na wala uhitaji utaalamu wa ziada kutambua hilo.

nadhani kwa biashara kama hii itabidi ulenge maeneo machache tu, mfano dar na arusha, ambako unaweza kupambana kufuatilia na kuhakikisha nakala feki chache zinaingia mtaani (huwezi zuia nakala feki zote) ambapo utajitahidi kurudisha faida (hii itategemea pia mikataba utakayowekeana na "outlets" zako). maeneo mengine itabidi tu uwe mpole na kuomba kwamba huko nakala feki hazishiki soko.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…