Naona kama Kombe La Dunia la mwaka huu halina 'mzuka'. Ni mimi peke yangu?

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
2,536
Reaction score
7,194
Wakuu,

Kombe la Dunia nimejulishwa ni mwezi wa 6 hapo lakini tofauti na miaka mingine kama 2010 au 2014 au 2018 ambapo miezi miwili au 3 kabla unaona kabisa kuna heka heka na shamrashamra lakini so far naona kimya

Sioni nyimbo za World Cup zikitrend. Nakumbuka kipindi kile kulikuwa na ule Wakawaka wa Shakira na wasanii mbalimbali walikuwa wanatoa nyimbo za World Cup lakin so far sijaona chochote

Lakini pia kunakuwaga na ofa mbalimbali zinatolewa na makampuni katika kipindi hiki. Utakuta kampuni za ndege, za simu au ving'amuzi vya TV vinakuwa na ofa lakini so far ni kimya

Lakini pia hata kwenye social media sioni watu wakizungumzia mambo ya World Cup.

Shida ni nin wakuu?
 
Ni kweli kabisa la mwaka huu mpaka sasa hakuna shamra shamra zozote kama sio mwaka wa kombe la Dunia labda mambo ya vita yamechangia
 
Iran Iran imekua maarufu imetufanya mpaka bei ya unga imepanda
 
Wakuu,

Kombe la Dunia nimejulishwa ni mwezi wa 6 hapo lakini tofauti na miaka mingine kama 2010 au 2014 au 2018 ambapo miezi miwili au 3 kabla unaona kabisa kuna heka heka na shamrashamra lakini so far naona kimya

Sioni nyimbo za World Cup zikitrend. Nakumbuka kipindi kile kulikuwa na ule Wakawaka wa Shakira na wasanii mbalimbali walikuwa wanatoa nyimbo za World Cup lakin so far sijaona chochote

Lakini pia kunakuwaga na ofa mbalimbali zinatolewa na makampuni katika kipindi hiki. Utakuta kampuni za ndege, za simu au ving'amuzi vya TV vinakuwa na ofa lakini so far ni kimya

Lakini pia hata kwenye social media sioni watu wakizungumzia mambo ya World Cup.

Shida ni nin wakuu?
Yote yamesababishwa na babu Trump. Baadhi ya nchi za ulaya zimetishia kujitoa hivyo mvuto um
Wakuu,

Kombe la Dunia nimejulishwa ni mwezi wa 6 hapo lakini tofauti na miaka mingine kama 2010 au 2014 au 2018 ambapo miezi miwili au 3 kabla unaona kabisa kuna heka heka na shamrashamra lakini so far naona kimya

Sioni nyimbo za World Cup zikitrend. Nakumbuka kipindi kile kulikuwa na ule Wakawaka wa Shakira na wasanii mbalimbali walikuwa wanatoa nyimbo za World Cup lakin so far sijaona chochote

Lakini pia kunakuwaga na ofa mbalimbali zinatolewa na makampuni katika kipindi hiki. Utakuta kampuni za ndege, za simu au ving'amuzi vya TV vinakuwa na ofa lakini so far ni kimya

Lakini pia hata kwenye social media sioni watu wakizungumzia mambo ya World Cup.

Shida ni nin wakuu?

Yote kayataka Trump.
Kuna nchi zinataka kujitoa km Spain
 
Tupo vitani mwaka huu hivyo tuna mpango wa kuarisha michezo yote
 
Mwaka umeanza na heka heka, maybe bado bado kidogo...kuna mambo yanatokea sasa hivi duniani ukiacha vita, kuna migawanyiko ya kijamii huko US, Europe hupelekea hata ule umoja kuanza kudorora...Haya yote yanasababishwa na Siasa za uongo.
 
Wewe hujaenda kwenye nchi zingine kwa hiyo labda unaongelea Tanzania ambapo yale mauaji ya halaiki yaliyotokea mwaka jana hayajatoka kwenye akili za wengi.

Hali hiyo imeathiri mambo mengi sana katika nchi hii kiasi kwamba watu wengi hawana furaha kabisa kwani watanzania walikuwa hawajawahi kushuhudia mauaji makubwa kama yale yakitokea nchini mwao, walikuwa wakiyasikia tu katika nchi zingine.
 
Back
Top Bottom